Na Amiri Kilagalila,Njombe
Sekretarieti ya Chama cha Mapinduzi CCM imewataka viongozi wa Chama hicho kutambua majukumu yao ili kiweza kuimarisha Chama.
Hayo yamebainishwa na katibu wa CCM Bi,Amina Imbo wakati wa ziara ya sekretarieti hii leo katika Jimbo la Lupembe kwa lengo la kuendelea kutoa maelekezo mahsusi ya chama katika ngazi za wilaya,kata,tawi na Shina.
Bi,Amina Imbo amewataka Viongozi wa kila ngazi kutambua majukumu yao katika nafasi zao wanazozitumikia ili kuendelea kukiimarisha chama katika nyanja zote huku pia akitumia ziara hiyo kutoa elimu juu ya Chanjo ya UVIKO -19
"Mimi Amina Imbo katibu wa CCM Mkoa wa Njombe nimechanja na sijapata madhara yoyote zaidi zaidi afya yangu imezidi kuimarika, tofauti na ilivyo kuwa mwanzo kabla ya kupata chanjo ya UVIKO- 19 pia katibu wa Siasa na Uenezi wa Mkoa wa Njombe amechanja na hakupata madhara yoyote"alisema Bi Amina
Naye katibu wa siasa na Uenezi wa Mkoa wa Njombe Erasto Ngole (Shikamoo Parachichi) ametumia jukwaa hilo kuwataka viongozi wote kusimamia zoezi endelevu la usajili wa wanachama wapya,Sambamba na ulipaji wa ada za uanachama, Pia amezitaka kata na Matawi yote yenye vitega uchumi kusimamia vitega uchumi ili kuondokana na dhana ya omba omba.
Aidha Ngole ametoa maelekezo kwa viongozi kuthamini na kutambua nafasi ya balozi katika Chama kwani ndiyo kiongozi pekee anayeishi na wanachama wake, ndiye anayetambua shida za wanachama wake kuliko kiongozi mwingine yeyote,Kupitia hilo Sekretarieti ya Mkoa imeshiriki kikao cha Mwenyekiti wa Shina namba Moja katika tawi la Lupembe.
ziara hiyo imehudhuriwa na katibu wa UVCCM Mkoa wa Njombe Cde Amosi Kusakula,Katibu wa UWT mkoa wa Njombe Bi.Frola Kapalia na Bi. Agatha Lubuva katibu wa wazazi mkoa wa Njombe.
Wakati huohuo Sekretarieti ya CCM mkoa wa Njombe imekagua ujenzi wa kituo cha afya Mtwango ambacho kinajengwa kwa kutumia mapato ya ndani,aidha Sekretarieti ya mkoa imetoa pongezi kwa Halmashauri ya Wilaya ya Njombe kwa kuendelea kusimamia fedha za miradi kama ilivyo desturi yao
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...