Jeshi la Polisi mkoa wa Njombe linawashikilia Raia Hamsini na moja wanaotajwa kuwa ni wahamiaji haramu kutoka nchi mbalimbali Ikiwemo Ethiopia na Malawi.

Raia hao wamekamatwa katika kijiji cha Igando halmashauri ya wilaya ya Wanging'ombe Kilomita  chache kabla ya kuingia Mpakani mwa mikoa ya Njombe na Mbeya.

Kamishna msaidizi wa Polisi Hamis Issa amekiri kuwashikilia raia hao na kueleza kwamba wamefanikiwa kuwakamata baada ya kupokea taarifa kutoka kwa wananchi wazalendo 

Issa ameongeza kuwa Raia hao walitelekezwa na Lori ambalo halijatambulika kwa haraka baada ya kutokomea nyakati za usiku baada ya kuwashusha raia hao walioeleza kutolewa Mkoani Tanga.

Jeshi la polisi mkoa wa njombe linaendelea na jitihada za kuutambua mtandao wa usafirishaji bin adam ikiwa ni pamoja na kuwafikisha mahakamani Raia hao zaidi ya Hamsini waliokamatwa kwaajili ya Hatua zaidi za Kisheria

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...