Muasisi wa Shirika la UNISHOP Tanzania Esther Mkaima akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na fursa kwa wanafunzi wa vyuo vikuu zinazotolewa na shirika hilo ikiwa pamoja na kupata punguzo la bidhaa katika maduka mbalimbali kupitia Programu ya 'Tambaa Nayo Program.' Leo jijini Dar es Salaam.




SHIRIKA La UNISHOP Tanzania limezindua kampeni ya 'Tambaa Nayo Program' maalumu kwa wanafunzi wa Vyuo vikuu kwa lengo kuwapunguzia gharama na kuwahudumia mahitaji yao ya kijamii, kielimu, afya na kiuchumi kwa gharama nafuu pamoja naa kuwatengenezea mazingira rafiki yatakayowawezesha kuyafikia malengo yao.

Akizungumza na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi huo leo jijini Dar es Salaam Muasisi wa Shirika hilo Esther Mkaima amesema, UNISHOP Tanzania ni jukwaa lenye malengo ya kuhakikisha wanafunzi wa vyuo vikuu wanapata mahitaji ya kijamii na kielimu kwa urahisi.

''Tunatengeneza mazingira rafiki kwa wanavyuo ambao watamiliki kadi za UNISHOP kwa gharama nafuu na zitawawezesha kupata huduma katika maduka ambayo tumeingia makubaliano nayo kwa punguzo la gharama isiyopungua asilimia 10 na kuendelea kwa hapa Dar es Salaam na programu hii ni maalum kwa vyuo vyote na katika ngazi zote...tutabandika vipeperushi katika maduka hayo na wanavyuo watapata huduma kwa punguzo kwa kuonesha vitambulisho vyao vya vyuo na kitambulisho cha UNISHOP.'' Amesema.

Pia amesema UNISHOP Tanzania wameandaa Program mbalimbali ikiwemo uwezeshaji kwa wanafunzi wa Vyuo Vikuu, Fursa na programu hiyo ya kuwarahisishia maisha wanafunzi wa vyuo vikuu kwa kuwapunguzia gharama katika matumizi yao ya kila siku wanapokuwa vyuoni kupitia maduka maalumu ambayo wanafunzi wa vyuo watatumia kadi maalumu na kupata huduma kwa punguzo la asilimia 10.

'' Lengo kuu la UNISHOP ni kuhakikisha wanavyuo wanapokuwa vyuoni wanatengenezewa mazingira rafiki yatakayowawezesha kufikia malengo yao kwa uhuru na wepesi bila changamoto zozote....Tupo hapa katika kuhakikisha wanavyuo wanapata mahitaji yao ya kijamii, kielimu, afya na kiuchumi.'' Amesema Esther.

Aidha amesema, kupitia programu za UNISHOP Tanzania wanavyuo watapata fursa ya kuwezeshwa kifikra, kiuchumi na kujitegemea na kupanga bajeti pamoja na kujisimamia katika nyanja za elimu, afya, kifedha na jamii katika maisha ya chuo na kuyatimiza malengo yao wakiwa kamili na tayari kwa mapambano ya dunia katika soko la dunia kwa kuajiriwa na kujiajiri.

Kwaupande wake Mwanachuo na Makamu wa Rais katika Serikali ya Wanafunzi ya Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM,) Philemon Mwakanyamale ameishukuru UNISHOP Tanzania kwa huduma walizoleta kwa wanafunzi hasa katika kuwapunguzia gharama katika maisha ya chuo.

Amesema, wanafunzi wa vyuo katika Mkoa wa Dar es Salaam watumie fursa hiyo katika kujijenga kimaarifa pamoja na kutembelea maduka ainishwa naa kupata huduma kwa gharama nafuu.


Mwanachuo na Makamu wa Rais wa Serikali ya Wanafunzi Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM,) Philemon Mwakanyamale (katikati) akizungumza wakati wa uzinduzi huo na kuwataka wanafunzi wote wa vyuo jijini humo kuchangamkia fursa hiyo adhimu itakayowasaidia katika maisha yao ya chuo, Leo jijini Dar es Salaam.


Muasisi wa Shirika la UNISHOP Tanzania Esther Mkaima (kulia,) akimkabidhi kadi maalumu ya UNISHOP Makamu wa Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM,) Philemon Mwakanyamale (kushoto) mara baada ya uzinduzi huo leo jini Dar es Salaam.


Makamu wa Rais wa Serikali ya wanafunzi ya Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM) Philemon Mwakanyamale akionesha kadi ya UNISHOP mara baada ya kukabidhiwa na muasisi wa shirika hilo Esther Mkaima leo jijini Dar es Salaam.



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...