Waziri
wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira
na Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama akihutubia wakati wa ufunguzi wa
kikao cha Kamati Elekezi ya Ulinzi wa Wanawake na Watoto katika Ukumbi
wa Hoteli ya Nashera Mkoani Morogoro tarehe 22 Oktoba, 2021.


Katibu
Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Dkt. Leonard Akwilapo
akichangia jambo wakati wa kikao cha Kamati Elekezi ya Ulinzi wa
Wanawake na Watoto, katikati ni Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Menejimenti
ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Dkt. Laurean Ndumbaro na kushoto ni
Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Christopher Kadio.

Baadhi ya wajumbe wa kikao cha Kamati Elekezi ya Ulinzi wa Wanawake na Watoto wakifuatilia kikao hicho.

Baadhi ya wajumbe wa kikao cha Kamati Elekezi ya Ulinzi wa Wanawake na Watoto wakifuatilia kikao hicho.

Waziri
wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira
na Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama, Katibu Mkuu wa ofisi hiyo Bw.
Tixon Nzunda (Kulia) pamoja na Katibu ya Kamati Elekezi ya Masuala ya
MTAKUWWA Bw. Sayi Magessa (kushoto) wakifuatilia kikao hicho.

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria Bw. Amon Mpanju akifafanua masuala ya kisheria wakati wa kikao hicho.

Waziri
wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira
na Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama pamoja na Makatibu Wakuu wakiwa
katika picha ya pamoja na sekretarieti ya Kamati ya Elekezi ya Ulinzi wa
Wanawake na Watoto.Kulia kwa waziri ni Katibu Mkuu wa ofisi yake, Bw.
Tixon Nzunda, kushoto kwake ni Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na
Teknolojia Dkt. Leonard Akwilapo, wa tatu kutoka kulia ni Katibu Mkuu
Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Christopher Kadio na wa tatu kutoka
kushoto ni Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na
Utawala Bora Dkt. Laurean Ndumbaro.
(PICHA ZOTE NA OFISI YA WAZIRI MKUU)
********************************
MWANDISHI WETU
Waziri
wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Sera, Uratibu,
Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama
ameitaka jamii kubadili mitazamo kwa kuhakikisha inapinga mila na
desturi zilizopitwa na wakati zinazokandamiza wanawake na watoto nchini.
Ameyasema
hayo alipofungua kikao cha Kamati Elekezi ya Ulinzi wa Wanawake na
Watoto kilichohudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Serikali, Wawakilishi
wa Mashirika ya Kimataifa,Wakuu wa Taasisi pamoja na Asasi za Kiraia
katika Ukumbi wa Hoteli ya Nashera Mkoani Morogoro mwishoni mwa wiki.
Waziri
alisema ni wakati sahihi kwa jamii kubadili mitazamo na kupinga mila na
desturi zinazowagandamiza wanawake na watoto na kupelekea kuathiri
katika maeneo mbalimbali..
“kumekuwepo
na mila na desturi potofu ndani ya jamii zetu zikiwemo za ukeketaji na
ndoa za utotoni ambazo zimeendelea kumkosesha haki na kuathiri maendeleo
na ustawi wa mtoto wa kike”alisisitiza.
Waziri
Mhagama alisema Serikali imeendelea kuweka mikakakti kuhakikisha
inatokomeza masuala ya ukatili dhidi ya Wananwake na Watoto nchini kwa
kupinga vitendo vya kikatili kwa makundi hayo pamoja na kuweka sheria na
kanuni zitakazoainisha namna bora ya kupambana na vitendo hivyo.
Aidha,
mila na desturi potofu zimechangia vitendo vya ukatili dhidi makundi
hayo ambapo vimechangia kukwamisha jitihada za kuelekea usawa wa
kijinsia na uwezeshaji wa wanawake hivyo zinahitajika jitihada endelevu
za pamoja baina ya serikali na wadau.
Alisema
yapo madhara mengi yatokanayo na vitendo vya ukatili kwa makundi hayo
ikiwemo kuwakosesha haki ya ushiriki katika shughuli za uzalishaji na
kujiletea maendeleo yao na jamii kwa ujumla.
.
“Wote
tunatambua madhara ya vitendo vya ukatili dhidi ya wanawake na watoto
kwa Taifa yakiwemo ya kiuchumi, kiafya na kijami,ukatili kwa watoto
hususan unaofanywa na watu au ndugu wa karibu umekuwa na athari mbaya
zaidi kwa ustawi na maendeleo ya watoto nchini,”alieleza waziri Mhagama.
Aliongezea
kuwa, katika kukabiliana na vitendo vya ukatili dhidi ya wanawake na
watoto hapa nchini serikali kwa kushirikiana na wadau imewezesha
uwanzishwaji wa madawati ya jinsia na watoto katika vituo vya polisi.
“Hadi
kufikia mwaka 2020/2021 jumla ya madawati 420 yameanzishwa katika vituo
mbalimbali vya polisi hapa nchini aidha jitihada za kukabiliana na
vitendo vya ukatili katika vyuo vya elimu ya juu na kati zimeendelea
ambapo hadi kufikia februari, 2021 jumla ya madawati matano ya jinsia
yameanzishwa katika taasisi za elimu ya juu na kati”, alisema.
Sambamba
na hilo alieleza katika kuimarisha ulinzi na usalama wa wanawake na
watoto nchini, jumla ya Kamati 18,186 za Ulinzi wa Wanawake na Watoto
zimeanzishwa katika ngazi ya Mkoa, Halmashauri, Kata na Kijiji/Mtaa
mwaka 2020/21 ikilinganishwa na Kamati 16,343 mwaka 2019/20, sawa na
ongezeko la Kamati 1,843.
“Nafahamu
Mpango wa Kutokomeza Ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto (MTAKUWWA)
unalengo la kupunguza ukatili kwa wanawake na watoto kwa asilimia 50
ifikapo mwaka 2021/22 ili kufikia lengo hilo serikali kwa kushirikiana
na wadau wa maendeleo imekuwa ikitekeleza afua mbalimbali zinazolenga
kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na watoto kupitia maeneo nane ya
utekelezaji”,amesema.
Waziri
aliendelea kuhimiza Kamati hiyo Kuhakikisha rasilimali fedha kwa ajili
ya utekelezaji wa afua za MTAKUWWA zinatengwa na kutolewa kwenye Wizara
na Taasisi husika, kuandaa mikakati madhubuti itakayosaidia kuimarisha
utendaji wa Kamati za Ulinzi wa Wanawake na Watoto kwenye ngazi zote na
Kuimarisha mifumo ya upatikanaji wa taarifa za ukatili nchini kwa lengo
la kubaini ukubwa wa tatizo na kulitafutia ufumbuzi stahiki.
Waziri
aliongezea kuwa ni vyema Kuendelea kubaini kada zenye upungufu mkubwa
wa watendaji hususan katika ngazi ya kata na vijiji ili kuwezesha
ufanisi katika utekelezaji wa mpango huo pamoja na kushughulikia
changamoto za sheria na kijamii zinazotoa mianya ya watuhumiwa wengi wa
kesi za ukatili kuachiwa huru.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...