WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ameshiriki katika mazishi ya aliyekuwa Mbunge Ngorongoro na Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu-Uwekezaji, William Tate Ole Nasha na amewasihi wananchi wamuenzi kwa kuyaendeleza mambo mazuri yote aliyoyafanya enzi za uhai wake.
 
Mheshimiwa Majaliwa ambaye ameshiriki katika mazishi hayo kwa niaba ya Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan amesema kifo cha Ole Nasha ni pigo kubwa kwa Serikali, Chama Cha Mapinduzi (CCM), Bunge pamoja na kwa wanafamilia na wananchi wa Ngorongoro.
 
Mazishi hayo ya Ole Nasha yamefanyika leo (Jumamosi, Oktoba 2, 2021) nyumbani kwake katika kijiji cha Osinoni kata ya Kakesyo wilayani Ngorongoro mkoa wa Arusha. Mbunge huyo alifariki Jumatatu, Septemba 27, 2021 mkoani Dodoma.
 
Waziri Mkuu amesema Mheshimiwa Rais Samia anawataka Watanzania waenzi mambo mazuri yote aliyoyafanya marehemu Ole Nasha ili jamii aliyokuwa anaiongoza inufaike. “Marehemu amefanya mambo mengi na ametoa mchango wa hali ya juu kwa Serikali.”
 
Amesema jambo la muhimu kwa sasa ni kuendelea kumuomba Mwenyezi Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema. “Mke wa marehemu, watoto, ndugu, jamaa na wabunge nawaombea kwa Mwenyezi Mungu awape moyo wa uvumilivu na subira katika kipindi hiki kigumu.

 





 

 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...