Na John Walter-Manyara

Waziri wa Kilimo Profesa Adolf Mkenda amesema gharama ya Kusafirisha mfuko mmoja wa mbolea wa kilogram 50 kwa njia yabarabara ni shilingi 55,000 hivyo wakala atakayeuza tofauti na hapo atakuwa ameenda kinyume na utaratibu.

Amesema bei hiyo ni kuanzia mbolea inapotolewa kutoka kiwandani adi mkoa mwingine bila kujali ni mkoa gani haipaswi kuzidi shilingi 10,000.

“Hatutarajii wakala yeyote anayeuza mbolea ya Nafaka Plus azidishe shilingi 65,000 hata akiwa pembezoni kabisa mwa nchi yetu” alisisitiza Waziri Mkenda

Waziri Mkenda amezungumza hayo leo ijumaa oktoba 8,2021 alipofanya ziara katika kiwanda cha Mbolea cha Minjingu wilayani Babati mkoani Manyara.

Pia Mkenda amesema mbolea ya kupandia tumbaku imeanza kuzalishwa katika kiwanda hicho ikiwa ni agizo la serikali ili kukabiliana na uhaba wa mbolea hiyo.

Serikali ya Tanzania kupitia Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea Tanzania (TFRA) hutumia fedha nyingi kuagiza mbolea nje ya nchi hivyo kuzalishwa kwa mbolea ya tumbaku na mbolea nyingine kwa wingi katika kiwanda hicho itasaidia kupungua kwa gharama hizo.

Amesema kuwepo kwa mbolea hiyo ambayo itasambazwa maeneo mabalimbali yanayozalisha tumbaku hapa nchini itasaidia pia kuongezeka kwa ajira hivyo kuongezeka kwa uchumi.

Mbolea hiyo ambayo ni (Nafaka Plus) inayotumika kwa ajili ya kuoteshea inasemekana kuwa na virutubisho vya ziada kuliko DAP.

Kwa upande wake mkurugenzi mtendaji wa Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea Tanzania (TFRA) Dr. Steven Ngairo amesema virutubisho vinavyopatikana katika Mbolea ya Minjingu ni nzuri na inafaa katika maeneo ambayo yana mvua nyingi.

Dr. Ngairo amesema kwa sasa mahitaji ya mbolea nchini Tanzania ni Laki saba ikiwemo tani laki moja na sitini za kupandia na laki mbili na ishirini mbolea ya kukuzia. Mkurugenzi wa kiwanda cha Minjingu Parbeep Hance amesema wapo tayari kuzalisha kwa wingi mbolea ili kuwasaidia wakulima kuzalisha mazao yao kwa wingi.


 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...