*Mpaka sasa, Kampuni imechangia zaidi ya $1M za kukabiliana na majanga
TANGU kuanza kwa janga la COVID-19, Meridian Gaming Group, moja ya kampuni kubwa inayojihusisha na michezo ya kubashiri imekuwa ikisaidia jamii kwenye maeneo yote inayofanyakazi. Imekuwa hivyo kwenye maonesho ya G2E, Las Vagas.
Siku ya hitimisha maonesho ya g2E, Meridian Group iliwasilisha matokeo ya
mchakato wa kukabiliana na janga la COVID-19 na kuonesha kuwa, ilichangia zaidi
ya $1M kwenye miradi inayohusiana na Covid ikiwa ni sambamba na kuyafikia
takribani majiji 150 barani Ulaya, LATAM na nchi za Kiafrika.
Wahudhuriaji wa maonesho ya gaming expo walivutiwa
zaidi na uhalisia kuwa, Meridian Group
ilijitolea vituo vyake vingi kuwa sehemu za kutolea chanjo kwenye maoneo mengi
duniani, sio tu kwa wafanyakazi wake bali kwa wananchi wote.
Kwa
zaidi ya miezi 18 sasa, Meridian
Gaming imeendelea kuzisaidia hospitali za
taifa, vituo vya afya, nyumba salama, vituo vya kuongezewa damu, mashirika ya
usawi wa jamii, mashirika ya afya yaliyopo Kusini Mashariki mwa Ulaya, Umoja wa
Ulaya, LATAM, Amerika ya Kati, Afrika na Asia.
Pia,
kampuni kwa kushirikiana na Shirika la Afya Duniani (WHO) walisaidia usambazaji
wa chanjo duniani, nafuu ya covid-19 na mpango wa kukabiliana na janga hilo.
Shukrani kwa kampuni kama Meridian,
WHO iliweza kuzisaidia nchi zilizoathirika zaidi kwenye jitihada zao za kampeni
ya kusambaza chanjo ya COVID-19.
Haijawahi kutokea, jamii zetu zimepitia majaribu makubwa na kwa sababu hiyo, Meridian imekuwa mfano wa kutukumbusha ushirikiano kote duniani ni njia sahihi ya kukabiliana na majanga.
Meridianbet, Nyumba Yenye Odds
Bora na Bonasi Kubwa!
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...