
Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari (WHMTH), Dkt. Zainab Chaula (kulia), akibadilishana hati na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Maulid Banyani baada ya kutiliana sahihi mkataba ambapo NHC itajenga jengo la ghorofa 6 la ofisi za Wizara hiyo kwa gharama ya zaidi ya sh. bilioni 23.9 katika Mji wa Serikali eneo la Mtumba jijini Dodoma katika hafla iliyofanyika leo Oktoba 8, 2021.

Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Dkt Chaula (kulia) na Mkurugenzi Mkuu wa NHC, Banyani wakitiliana saini mkataba wa makubaliano ya ujenzi huo, huku Waziri wa wizara hiyo, Dkt Ashatu Kijaji (aliyevaa miwani mieusi) akishuhudia.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari (WHMTH), Dkt. Zainab Chaula (kulia), akibadilishana hati za mkataba na Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Nyumba za Serikali (TBA), Daud Kondoro baada ya kutiliana saini mkataba huo ambapo TBA watakuwa wakandarasi washauri wa ujenzi huo.Wanaoshuhudia katikati ni Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Dkt Ashatu Kijaji na Meshack Bandawe ambaye ni Katibu wa Kuhamishia Serikali Dodoma na Mratibu wa Ujenzi wa Mji wa Serikali.

Waziri Dkt Kijaji na Katibu Mkuu wa wizara hizo, Dkt Chaula wakikagua kiwanja patakapojengwa jengo la wiyara hiyo.

Katapila likisawazisha sehemu ya kiwanja hicho tayari kwa kuanza ujenzi.

Baadhi ya maafisa wa wizara hiyo wakihudhuria hafla hiyo.

Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Dkt Chaula akizungumza kabla ya kumkaribisha Waziri Dkt Kijaji kuzungumza wakati wa hafla hiyo.

Ofisa Mtendaji Mkuu wa TBA, Daud Kondoro akizungumza wakati wa hafla hiyo huku akiahidi watahakikisha kazi waliyopewa wanaitekeleza kwa muda na ubora unaotarajiwa.

Mkurugenzi Mkuu wa NHC, Dkt. Banyani akielezea jinsi walivyojipanga kuanza kazi ya ujenzi wa jengo hilo huku akiahidi kuikamilisha kwa muda uliopangwa wa miaka miwili au chini yake na kwa ubora unaotakiwa.

Dkt Banyani wa NHC akisisitiza jambo.

Meshack Bandawe ambaye ni Katibu wa Kuhamishia Serikali Dodoma na Mratibu wa Ujenzi wa Mji wa Serikali. akiipongeza wizara hiyo kwa kuanza ujenzi mapema na kuahidi kusimamia ipasavyo ili ujenzi huo na majengo mengine ya wizara takribani 24 unakamilika kwa muda uliopangwa na ubora unaotakiwa lakini pia kuhakikisha miundombinu yote inakamilika.

Waziri Dkt Kijaji, akizungumza kabla ya shughuli ya kutiliana saini mikataba kuanza ambapo amewataka Mkandarasi wa Jengo hilo, Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) na Wakala wa Nyumba za Serikali (TBA), washirikiane kuhakikisha ujenzi unaanza mara moja, wajenge kwa ubora unaotakiwa na kukamilisha ujenzi kwa muda uliopangwa na hata chini ya hapo.
Waziri Kijaji amemshukuru Rais wa Awamu ya Sita, Samia Suluhu Hassan kwa kutoa fedha ya kujengea majengo ya wizara ikiwemo ya kwao, na kwamba kwa upande wao wameamua kuanza mchakamchaka wa ujenzi wa jengo lao na watakuwa wanafanya zamu ya kufuatilia ujenzi huo kila siku asubuhi, mchana na jioni.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...