Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Ndg. Daniel Chongolo amesema ni lazima Chama kishikane mashati na serikali ili kutimiza kile kichohiahidi kwa wananchi wake.

Ndg. Chongolo ametoa kauli hiyo leo tarehe 22 Novemba 2021 kata ya Simbo Wilaya ya Igunga Mkoani Tabora alipofika kufanya ziara ya siku mbili kukagua utekelezaji wa ilani na kuhimiza uhai wa chama ngazi ya mashina.

“Sisi tulichoahidi hatuko tayari kuwa waongo, ni lazimi tushikane mashati kutimiza kile ambacho tuliahiadi na hiyo ni kazi ya CCM na Mwenyekiti wa CCM na Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan amenituma kufanya hapa,” Katibu Mkuu ameeleza.

Katibu Mkuu amesema hayo baada ya kupata malalamiko ya Mbunge wa jimbo la Manonga wilaya ya Igunga Ndg. Seif Gulamali akiilaumu serikali kutojenga barabara ya Ndala-Simbo-Nkinga-Ziba mpaka Shinyanga vijijini, kwa muda mrefu huku waziri wa ujenzi akiwaambia kuwa atafikiria endapo hiyo barabara itajengwa.

Ndg. Chongolo amesema kuwa, Waziri huyo hatakiwi kufikiria kutenda na kwamba ni wajibu wake kutenga fedha kwa ajili ya ujenzi na kutekeleza Ilani ya chama.

“Hatutaki Waziri afikirie, ni wajibu wake kutenga fedha kwa ajili ya ujenzi na utekelezaji wa Ilani,” amesema na kuongeza kuwa, Waziri anayefikiria kutimiza wajibu wake hana uhakika, huku akisisitiza kuwa Waziri anatakiwa kuwajibika kutimiza wajibu wake kwa sababu chama kilishaahidi mwaka 2020 na ndani ya miaka mitano ni lazima kitekeleze.

Katibu Mkuu amewaeleza wananchi kuwa akirudi ofisini kwake atamtaka waziri ampe mpango wa utekelezaji wa barabara hiyo ili iweze kujengwa kwa kuanzia mwaka ujao wa fedha wa 2022/2023.

Aidha, Katibu Mkuu amesema Mawaziri wote wanatakiwa kutekeleza Ilani bila kufikiria huku akitaja uunganishwaji wa umeme wa REA vijijini kama sehemu nyingine ya utekelezaji wa Ilani unaiyumba wilaya ya Igunga

“Nimeona umeme hapa, nitarudi na kumuuliza waziri wa nishaiti mpango wa kuhakikisha mwakani mwezi wa kumi na mbili vijiji vyote vya jimbo la manonga na Tabora yote vinatapa umeme , kwa sababu hiyo ndiyo ahadi ya CCM na inatakiwa itekelezwe na serikali,” Katibu Mkuu Ndg. Chongolo amesisitiza

Katibu Mkuu amesisitiza kuwa wamekubalina na kuweka mpango kwamba vijiji vyote Tanzania ifikapo disemba, 2022 lazima viwe vimepata umeme.

Amesema CCM ikiacha mawaziri wafanye kwa kufikiria, watavuka kipindi hicho umeme haujafika na kwamba wao waliahidi na wao wamekabidhi jukumu la kutenda walichoahidi kwa serikali ni lazima wasimamie utekelezaji wake.








Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...