kampuni inayoongoza ya mfumo wa usafiri wa kukodi barani Afrika, imezindua huduma ya Boda-boda jijini Dodoma katika jitihada zake za kurahisisha upatikanaji wa huduma za usafiri nchini Tanzania.
Huduma ya Bolt Boda inawapatia wasafiri njia mbadala
ya kusafiri, ikiongeza ukuaji wa huduma za usafiri wa kukodi
zinazopatikana sokoni kwa sasa. Huduma hii vile vile inakusudia kuleta
huduma za usafiri za uhakika na za bei nafuu za Bolt karibu na wateja
wakati huo huo ikiwa inaimarisha upatikanaji wa huduma zake hapa nchini.
“Tunaendelea
kuongeza wigo wa huduma zetu kwa manufaa ya wateja wetu na kuwekeza
rasilimali katika huduma zenye ubora ambazo zinakidhi mahitaji ya jamii.
Pikipiki ni moja kati ya njia ya haraka zaidi ya kutoka sehemu moja
kwenda nyingine ndani ya jiji la Dodoma, na tunashauku ya kuwapatia
wateja wetu njia mbadala na nafuu ya kwenda sehemu mbalimbali ndani ya
jiji,” Alisema bwana Remmy Eseka, Meneja wa Bolt Nchini Tanzania.Uzinduzi
huu wa huduma ya safari ya Bolt Boda unaleta mtandao unaokuwa kwa kasi
wa usafiri wa Bolt kwa njia ya boda boda kwenye miji mitatu nchini
Tanzania ikiwemo Dar es salaam, Mwanza na Dodoma.
Kampuni
ya Bolt inatoa fursa mbalimbali za huduma za usafiri wa kukodi kwa
gharama nafuu sokoni na inaendelea kuwa na ukuaji imara ambao
unaendeshwa na mahitaji ya huduma zake za bei nafuu na zenye ubora.
Huduma
ya Bolt BODA ni huduma nyingine ya nyongeza katika orodha ya huduma
mbalimbali inayotolewa na Bolt, ikiwemo huduma ya Bolt Base na Bolt Lite
kwaajili ya kuhudumia mahitaji ya kipekee ya wasafiri wa Dodoma.
Wateja
wanaweza kupata huduma ya Bolt BODA kwa kupitia kwenye App ya Bolt kwa
gharama nafuu ya TSZ 1,000. Gharama ya TZS 220 kwa kila kilomita moja,
gharama ya TZS 50 kwa dakika na nauli ya msingi ya TZS 600. Madereva wa
Bolt watabakiwa na 80% ya mapato yao na bolt itawatoza ada ya asilimia
20% kwa kila safari, ambayo inaweza kulipiwa kwa kadi au fedha taslimu.
Kampuni
ya Bolt itasajili waendesha boda-boda wenye vitambulisho vya Taifa,
leseni ya udereva, cheti cha polisi cha ithibati, leseni ya vyombo vya
usafiri LATRA, kadi ya usajili ya gari (usajili wa kibiashara) na bima
ya vyombo vya usafiri. (Kibiashara).
“Biashara yetu kubwa ni
kutoa huduma ya usafiri ya uhakika, salama na ya bei nafuu kwa kila
mmoja, na tunashauku ya kufanya huduma ya usafiri iwe rahisi zaidi, ya
haraka nchi nzima katika kipindi hiki cha sikukuu”. Alisema Remmy.
Kuhusu Bolt
Bolt
ni kampuni ya mfumo wa usafiri yenye asili ya Ulaya inayoongoza ambayo
imedhamiria katika kufanya usafiri wa maeneo ya mijini kuwa wa gharama
nafuu, rahisi na wenye ufanisi.
Kampuni ya Bolt ina zaidi ya
watumiaji milioni 50 katika zaidi ya nchi 40 katika bara la Ulaya na
Afrika. Huduma zake zinajumuisha usafiri wa kukodi, kwa wasafirishaji
wadogo wadogo wenye pikipiki ndogo na baiskeli za kutumia umeme pamoja
na usafirishaji wa vyakula na vifurushi.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...