Khadija Kalili: Na Khadija Kalili, Chalinze
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi  (CCM) Wilaya ya Bagamoyo Mkoani Pwani   Alhaj Abdul Sharif amewapongeza wadau wa elimu Jimbo  la  Chalinze  huku akitoa rai kwa Halmashauri ya Chalinze kuwaunga mkono  katika juhudi zilizoonyeshwa na  jukwaa hilo katika  kupandisha kiwango cha elimu.
Akizungumza kama mgeni rasmi kwenye Kongamano hilo la lililoandaliwa na wadau wa elimu Chalinze  Mwenyekiti huyo alisema kuwa wakati umefika  kwa wana Chalinze kujitathimini  kwa kina hali ya kiwango cha  elimu ilivyo hivi sasa hasa kwa wanafunzi wa shule za msingi na sekondari  kufuatia  kudorora kwa kiwango cha elimu kwa ujumla.
 "Kwa mujibu  wa takwimu kimazingira  inaonyesha kuwa  Chalinze ndani ya kipindi  kati ya 2015 na 2020  wanafunzi wengi wamekua hawafanyi vizuri katika elimu ya msingi na sekondari ambapo wamekuwa wakikabiliwa na changamoto mbalimbali ndani na nje ya familia  zao ambazo endapo tukiunganisha nguvu zetu kwa  pamoja nina imani kubwa vijana wetu watashika madaraja ya juu katika kiwango cha elimu"alisema Alhaj Sharif.
Alisema kuwa wazazi na viongozi wote kwa pamoja  wanajukumu la kutathmini  juu ya mfumo  mzima wa elimu namna ya ufundishaji kitafuta mbinu za kumwezesha mwanafunzi kuweza kuelewa masomo na kuwa na ari ya kusoma  sambamba na wazazi kuwafuatilia watoto wao waendapo na kurudi kutoka shuleni.
"Hivi Sasa idadi  ya vijana  wa Chalinze wanaokwenda  katika shule za  vipaji ni wa chache  hii ni tathmini ya mwaka 2016 na 2021  hivyo  aliwaambia wanaJukwaa pamoja na wadau waliojitokeza kuhudhuria Kongamano Hilo la elimu kuwa  wanapaswa kuto kata tamaa kutokana na  changamoto mbalimbali walizozipitia" na zilizo jitokeza kala ya kufanyika kwa Kongamano hilo.
"Kupitia jukwaa hili  la Wadau wa Elimu Chalinze litaweza   kuatua  mambo mengi  kielimu sababu elimu ndiyo kila kitu katika maisha " alisema Shariff.
"Tupo  hapa kujadili mustakabali wa elimu  na mimi binafsi nawaaahidi kwamba  nitakuwa bega kwa bega na nyinyi muda wowote na salaamu za jukwaa hili nitazioeleka panapostahili ikiwemo kuzungumza moja kwa moja na Mheshimiwa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan kuwa kuna jukwaa ambalo linaundwa  n watu makini wenye uchungu na Chalinze" alisema Mwenyekiti huyo.
"Suala la elimu liko ndani ya Ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) nasisitiza  Halmashauri  ya Chalinze kwa pamoja na jukwaa waweke mikakati madhubuti itakayopandisha kiwango cha elimu   ikiwemo kutoa hamasa kwa  waalimu kuwekewa mazingira rafiki ya kufundisha"Afisa Mipango Halmashauri ya Chalinze Shaban Milawoalisema kuwa  wataanzisha utaratibu kwa Kamati ya Ulinzi na  Usalama kufuatilia mahudhurio ya wanafunzi mashuleni ikiwa ni katika kupambana na tabia ya utoro pia wataje ga  nyumba za waalimu ikiwa ni katika kutoa hamasa ya kufundisha.
Jukwaa  hilo la Wadau wa Elimu Chalinze liliasisiwa   na  watu wa kada mbalimbali miaka saba iliyopita pia limehudhuriwa na watu mbalimbali ikwemo, waalimu , vijana na  baadhi ya Madiwani wa Jimbo hilo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...