Na Amiri Kilagalila,Njombe
Wakulima 10,968 wa mkoa wa Njombe wanatarajia kunufaika na pembejeo kwa njia ya mkopo kupitia kampuni ya Ekari moja Tanzania (One Acre Tanzania Limited) kwa msimu wa kilimo wa mwaka 2021-2022 kwa kupata fursa ya kulipa kidogo kidogo mkopo huo.
Kampuni hiyo kwa msimu wa mwaka 2021-2022 imefanikiwa kutenga fedha kiasi cha zaidi ya Shilingi Bilioni Tatu ili kutoa pembejeo za mkopo kwa wakulima waweze kulima kwa tija ambapo pia wakulima wameshauriwa kupanda mbegu za mazao ya muda mfupi kutokana na mabadiliko ya hali ya hewa.
Akitoa taarifa namna wananchi wa mkoa wa Njombe watakavyo nufaika na mkopo wa pembejea hizo wakati akikabidhi pembejeo za mkopo kwa wakulima wa kijiji cha Matembwe halmashauri ya wilaya ya Njombe,afisa mahusiano wa kampuni na serikali Bi. Neema John amesema zaidi ya wakulima elfu kumi wanaenda Kunufaika na mkopo huo.
“Tunaendelea kushirikiana na wiazara ya kilimo katika kuimarisha huduma za ugani kwa kushirikiana kwa ukaribu na wataalamu wa kilimo na huduma za ugani katika maeneo tunayofanyia kazi”alisema Bi,Neema John
Amongeza kuwa “Kwa msimu huu wa 2021-2022 kampuni imewekeza zaidi bilioni tatu milioni mia nne na arobaini na sita,laki saba na elfu nane na mia nane kwa wakulima elfu kumi na mia tisa stini na nane wa mkoa wa Njombe”alisema afisa mahusiano wa kampuni
Kuhusu eneo la wilaya ya Njombe ambako ilikuwa ikifanyika shughuli ya kugawa pembejeo hizo amesema “Wilaya ya Njombe imebeba kiasi cha uwekezaji wa shilingi milioni mia nane sabini na tisa,laki tisa na kumi na mia saba ili kuhudumia elfu tatu mia tatu na stini na moja kwa njia ya mkopo kupitia mradi mkuu,tumeanza usambazaji wa pembejeo na tunatarajia kusambaza zaidi ya tani mia nne hamsini point tano tano za mbolea na tani tatu za mbegu”
Mkuu wa wilaya ya Njombe Kissa Kasongwa amewataka wakulima kufuata maelekezo ya wataalamu ili kuzalisha kwa tija.
“Ukichelewa kuweka mbolea kwenye shamba lazima utapunguza ubora wa matokeo ambayo unayatarajia na ndipo azma ile ya One Acre Fund ya vuna zaidi itakpokosekana,lakini tukifuata maelekezo ile azma tutaiona kwa haraka”alisema Kissa
Kwa upande wake katibu tawala wilaya ya Njombe Emmanuel George wamewataka wakulima kupanda mazao ya muda mfupi kutokana na mabadiliko ya hali ya hewa huku wananchi wa kijiji hicho wakifurahi kupata mkopo huo,
“Lakini ile faida iendeleze kilimo ulichonacho lakini pia na wewe kikufanye utoke kwenye hatua moja kwenda nyingine na hicho kilimo kinahitaji kusikiliza sana masharti na vigezo ambayo wataalamu wanatueleza kwasababu sasa hivi kuna mabadiriko sana ya hali ya hewa”alisema Emmanuel.
Mkuu wa wilaya ya Njombe Kissa Kasongwa akikabidhi mbolea iliyotolewa na kampuni ya One Acre kwa wakulima wa kijiji cha Matembwe.

Mbolea zilizofika katika kijiji cha Matembwe wilayani Njombe kwa ajili ya kuwafikia wakulima wa kijiji hicho.
Afisa mahusiano wa kampuni na serikali wa shirika la One Acre Fund Bi. Neema John akitoa taarifa ya namna mradi utakavyotekelezwa katika mkoa wa Njombe kwa mwaka 2021 -2022
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...