Na Amiri Kilagalila,Njombe

Ili kujikwamua kiuchumi kuanzia ngazi ya familia na kuepuka utegemezi,wanawake wa Chama cha Mapinduzi wilayani Wanging’ombe mkoani Njombe wamepewa elimu ya ufugaji wa kuku wa kienyeji kwa njia kisasa utakaowawezesha kupiga hatua kiuchumi.

Akizungumza wakati wa semina ndogo ya ujasiriamali iliyofanyika katika ukumbi wa kanisa katoriki,mwenyekiti wa jumuiya ya umoja wa wanawake Tanzania (UWT) Scolastika Kevela ametoa wito kwa wanawake wa Chama hicho kuwa na wivu wa maendeleo kwa kuwa kuku ni ukombozi wa uchumi.

“Tuwe na wivu wa maendeleo,kuku ni mkombozi wa uchumi wetu,akina mama tukijikomboa kiuchumi tutakuwa tumekomboa taifa zima kwa ujumla na hata mimi nimefuga nyumbani kwangu”alisema Scolastika Kevela

Mwenyekiti amebainisha kuwa kuku mmoja ana uwezo wa kuleta zaidi ya kuku zaidi ya 3000 kwa mwaka mmoja endapo akitunzwa na kuwaomba akina mama kuanza kuchangamkia fursa ya ufugaji huo usio umiza.

“Tetea watano wanakuletea kuku 900 kwa mwaka ina maana ndani ya miezi miwili kukuku mmoja anaweza akakuletea vifaranga 30,vifaranga 30 ndani ya mwezi ukizidisha kwa kuku watano watakupatia vifaranga 372 lakini kwa miezi 12 utapata 4500 hapa tumeondoka kwenye umaskini”amesema mwenyekiti

Aidha ili kufanikisha adhma hiyo ya kujikomboa kiuchumi kwa wanawake wa wilaya hiyo,mwenyekiti amefanikiwa kuanza kwa kuwakabidhi kuku watano kila tarafa katika tarafa tatu za Mdandu,Wanging’ombe pamoja na Imalinyi watakaofugwa kwa kikundi huku akiwahakikishia uwepo wa soko la kutosha la kuku endapo akina mama hao wakifanikiwa kufika malengo ya ufugaji.

Nao baadhi ya akina mama wa Tarafa hizo wamemshukuru mwenyekiti kwa elimu na msaada huo utakaokwenda kuwafungulia uchumi kwa kuanza na mtaji mdogo wa kuku waliokabidhiwa.

Licha ya akina mama wa tarafa hizo kukabidhiwa mtaji huo wa kuku lakini pia mwenyekiti huyo amefanya hivyo kwa tarafa za wilaya ya Makete na Ludewa alipofika na kamati ya utekelezaji ya UWT mkoa wa Njombe katika wilaya hizo kukagua miradi ya maendelo na uhai wa jumuiya.

Picha ya Mtandaoni ikionyesha namna kuku wa kienyeji wanavyofugwa kisasa.

Mwenyekiti wa jumuiya ya umoja wa wanawake Tanzania (UWT) Scolastika Kevela akitoa rai kwa wanawake kuanza ufugaji wa kuku wa kienyeji kwa njia ya kisasa ili waweze kujikwamua kiuchumi.
Baadhi ya wanawake wakisikiliza maagizo ya kamati ya utekelezaji mkoa wa Njombe mara baada ya kupewa elimu ya ujasiliamali wa ufugaji wa kuku kwa njia za kisasa.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...