KATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Daniel Chongolo amezitaka familia zenye watoto wenye ulemavu kuacha kuwaficha Kwa Imani potovu kuwa watoto hao ni laan kwenye famili hizo na badala yake wawajibike kuwatimizia haki zao ikwemo kuwapeleka shule.
Chongolo ametoa Rai hiyo Leo wakati akiongea na wananchi wa Kata ya Igunga Wilaya ya Igunga Mkoani Tabora. Amesema baadhi ya familia haswa Mkoani Tabora wanaficha watoto wenye ulemavu wakiamini kuwa ni laana na kushindwa kuwapa stahiki zao.
Amelaumu familia ambazo zinaficha watoto wenye ulemavu na kushindwa kuwanyima fursa ya Elimu, kumpeleka hospital wakiwachukulia kama Sio watoto Sawa na wengine.
Amesema ni lazima familia zitambue kuwe watoto wenye ulemavu ni binadamu wenye kustahiki ya kutendewa haki Sawa na wengine, wapelekwe kusoma na kupewa matibabu wanapohitaji kwani kila mttoto anakipaji chake ambacho amepewa na Mungu.
Amesema mtoto mwenye ulemavu akiwezeshwa wanaweza kufanya Maajabu huku akisisitiza familia zenye watoto wenye ulemavu kuwapa fursa kuwalea, na kuwasaidia kufikia malengo Yao ambayo Mungu amewapangia ambapo kwa kuwa kuna vyuo vya ufundi pia wanaweza kusoma ufundi na wakawa na uweledi wa fani mbalimbali na kuendesha maisha yao.
Aidha katika hatua nyingine, chongolo amevitaka vyuo vya Ufundi (VETA) kuhakikisha vinajenga vyuo vyao wenyewe na sio kuwapatia watu ama taasisi nyingine kujenga vyuo hivyo kwa sababu wao wananguvu kazi zaidi na wanaweza kutumia miradi hiyo kama sehemu ya vijana wao kujifunza kwa vitendo.
Ameeleza hayo alipotembelea na kukagua maendeleo ya mradi wa ujenzi wa chuo cha veta Igunga ambacho kinajengwa na Veta wenyewe, ambapo chongolo amefurahishwa na maendeleo ya ujenzi wa chuo hicho kinachogharimu shilingi bilioni 2.2 na kinatarajiwa kukamilika mwezi februari, 2022.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Daniel Chongolo akimsikiliza Mbunge wa Jimbo la Igunga
Nicholaus Ngassa
(mwenye kofia) wakati wa ukaguzi wa mradi wa maji Igunga unao wahudumia watu 66,186 wa Igunga. (Picha na CCM Makao
Makuu)
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Daniel Chongolo akiwa juu ya tenki la maji
lenye uwezo wa kuhudumia watu 66,186 wa Igunga. (Picha na CCM Makao
Makuu)
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Daniel Chongolo akihutubia wakazi wa shina namba 20 lililopo kata ya Igunga , Igunga mkoa
wa Tabora. (Picha na CCM Makao Makuu)
Katibu Mkuu wa CCM
Ndugu Daniel Chongolo akiwa na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Tabora wakati
wa kikao cha shina namba 7lililopo Mbutu, Igunga mkoa wa Tabora. (Picha
na CCM Makao Makuu)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...