Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini Mh. Anthony Mavunde amewataka wanafunzi wa kidato cha IV wa Shule za Sekondari Jijini Dodoma wanaotarajia kufanya mitihani yao ya Taifa Novemba,2021 kuongeza juhudi na umakini ili kulipaisha Jiji hilo kitaaluma

Mavunde ameyasema hayo wakati wa sherehe za mahafali ya kidato cha IV za Shule ya Sekondari Mlimwa Jijini Dodoma na kutumia fursa hiyo kuwahamasisha wanafunzi hao kufanya vyema katika mitihani yao.

“Najua mmefanya maandalizi ya kutosha mpaka kufikia hatua hii,na naelewa vyema kuwa walimu wenu wamejitahidi kuwaandaa vizuri kwa ajili ya mitihani hii ya mwisho ya kitaifa.

Kwa muda huu mchache uliobakia tuongeze juhudi na umakini ili tuweze kufanya vizuri zaidi na kuiletea heshima Dodoma kutokana na matokeo yetu mazuri.

Nawaombea kwa Mwenyezi Mungu awatunze na kuwalinda na awajaalie kheri na maarifa ya kutosha wakati mkiwa mnaanza mitihani yenu”Alisema Mavunde

Aidha,akijibu Risala ya wanafunzi,Mh Mavunde ameishukuru serikali chini ya **Mh Rais Samia Suluhu Hassan **kwa ujenzi wa madarasa matatu shuleni hapo,ambapo pia Mbunge Mavunde alitumia fursa hiyo kukabidhi Computer 1, viti vya walimu 30,magoli ya chuma kwa ajili ya uwanja wa michezo shuleni sambamba na jezi na mipira.

Akitoa shukrani kwa niaba ya Wanajumuiya wa Sekondari ya Mlimwa,Diwani wa kata ya K/Ndege Mh Amos Mbaranga ameishukuru serikali pamoja na Mbunge Mavunde kwa jitihada kubwa za kuendeleza sekta ya Elimu na kuahidi kusimamia kwa dhati shughuli zote za maendeleo shuleni hapo.






Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...