Mganga Mkuu wa mkoa Dar es Salaam Mfaume Rashid akitoa Elimu ya corona katika Mkutano Mkuu wa Jumuiya ya Wazazi Mkoa wa Dar es Salaam.
Viongozi waJumuiya ya Wazazi Mkoa wa Dar es Salaam na Taifa wakiwa katika picha ya pamoja katika mkutano Mkuu wa Jumuiya hiyo leo Dar es Salaam.
Mjumbe wa Kamati ya Utekelezaji  Wazazi Mkoa wa Dar es Salaam Habibu Nassar akiwa katika ukumbi wa Karimjee Dar es Saalam leo katika mkutano wa Jumuiya ya Wazazi Mkoa wa Dar Es Salaam  (kushoto)Diwani wa Kata ya Kisutu Sharik Chougule.




NA HERI SHAABAN

JUMUIYA ya Wazazi Tanzania wametakiwa kushikamana kuwa wamoja katika kutetea chama cha mapinduzi kushika dola .

Hayo yalisemwa na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Taifa   Edmundi Mndolwa katika mkutano Mkuu wa mkoa wa Jumuiya hiyo uliofanyika leo  Wilayani Ilala .

"Nawaomba wana Jumuiya ya Wazazi wote nchini kushikamana kujenga chama na Jumuiya yetu kwa dhumuni la kushirikiana kuakikisha chama kina shika dola " alisema Mndolwa.

Mwenyekiti Mndolwa alisema jukumu la kwanza la Jumuiya ya Wazazi kuakikisha kinatetea chama kiweze kushika dola  na kuibuka na ushindi mnono katika chaguzi mbalimbali.

Mndolwa alisema Jumuiya ya Wazazi ni JUMUIYA Tajiri kushinda jumuiya zote na mikakati yake imejiwekea kila kaya kupanda miti mitano ambapo itasaidia huko mbele nchi kupata fedha nyingi .

Aliwagiza Wenyeviti wa Mkoa wa JUMUIYA ya Wazazi kuiga mfano wa jumuiya ya Wazazi Mkoa wa Dar es Salaam kwa kufanikisha mkutano mkubwa


Wakati huo huo Mwenyekiti Mndolwa alisema hivi karibuni Makatibu wote wa mikoa Tanzania watatangzwa Wajumbe wa Baraza ndani ya Jumuiya ya Wazazi.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Mkoa wa Dar es Salaam Frank Kamgisha  amewataka wanaccm wa jumuiya hiyo waache tabia ya kupanga safu ya wagombea kwani kampeni bado hazijaruhusiwa.

Naye Katibu wa CCM Mkoa Adam Ngalawa aliwataka wana CCM kuondoa makundi ndani ya chama kwani si wakati wake kwa sasa badala yake amewataka wana CCM kujenga chama .


Mganga Mkuu wa Mkoa Mfaume Rashidi  amepongeza wana CCM kuchanja chanjo ya corona 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...

Back To Top