Na Amiri Kilagalila,Njombe
Wakazi wa kijiji cha Itambo kata ya Mdandu wilaya ya Wanging'ombe mkoani njombe wameondokana na changamoto ya gharama kubwa na kusafiri umbali mrefu kwenda kufuata huduma ya kukoboa na kusaga nafaka baada ya jumuiya ya wanawake Tanzania (UWT) wilayani humo kuzindua rasmi mradi wa mashine ya kukoboa na kusaga nafaka katika kijiji hicho.
Mwenyekiti wa UWTt mkoa wa Njombe Scolastika Kevela amesema jitihada za viongozi mbalimbali akiwemo katibu wa siasa na uenezi CCM mkoa wa Njombe Erasto Ngole zimesaidia sana kufanikisha mradi huo huku mjumbe wa baraza la wanawake ccm taifa mkoa Anna Mwalongo akitaka wanawake wa Wanging'ombe kuutunza mradi huo ili uwaongezee kipato.
“Unapokuwa kiongozi wa mkoa hatuiangalii Wangi’ombe tu,huyu kiongozi anazunguka mkoa mzima kwa kweli sisi UWT tunamshukuru sana Mwenezi,leo tumepata kiwanda hiki kidogo ili kuinua uchumi wetu tunaomba mkitunze”alisema Scolastika Kevela
Taarifa ya mradi huo iliyosomwa na kaimu katibu wa UWT wilaya ya Wanging'ombe ambaye ni diwani wa viti maalum tarafa ya Mdandu Vumilia Kilamlya imeeleza kuwa hadi kukamilika kwake umetumia zaidi ya shilingi milioni sita.
Akizindua mradi huo katibu wa siasa na uenezi CCM mkoa wa Njombe Erasto Ngole ametaka jitihada hizo zioneshe matokeo chanya ili waweze kupewa motisha zaidi huku akionya suala la migogoro ndani ya jumuiya hiyo kauli iliyoungwa mkono na mwenyekiti wa UWT wilaya ya Wanging'ombe bi. Christina Sanga.
“Nitataka hesabu za kipindi cha mwaka mmoja ili nione kama mashine imezalisha vizuri na kwamba sasa mnastahili kupata Piki Piki,kwasababu palipo na akina kuna maneno, nah ii mashine pia inaweza ikawafarakanisha kwa hiyo tuwachugue watu wachache wenye uchungu waisimamie mashine yetu”alisema Erasto Ngole
Wakizungumza baada ya kuzinduliwa kwa mradi huo baadhi ya wakazi akiwemo Edina Mwagala na Tumain Ngilangwa wanakiri kuwa sasa adha ya kutembea umbali mrefu kwenda kufuata huduma ya unga itapungua kwa kuwa mashine moja iliyokuwapo ilikuwa na foleni ndefu na pindi inapoharibika mateso ndipo yanapoanza.
Mradi wa mashine ya kusaga na kukoboa unatajwa kwenda kuwainua wanawake hao kiuchumi endapo watauendeleza vyema.
Katibu wa siasa na uenezi mkoa wa Njombe Erasto Ngole akiweka mahindi kwenye mashine kuonyesha ishara ya mashine hiyo kuanza kufanya kazi rasmi.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...