Na
Mwandishi wetu- MOI
Taasisi
ya Tiba ya Mifupa Muhimbili (MOI) imesaini mkataba wa ushirikiano na Chama cha
Madaktari China (CMA) pamoja na hospitali ya Tian Tan kwa lengo la kuboresha huduma
za kibingwa hapa nchini.
Hayo
yamesemwa na Mkurugenzi Mtendaji wa MOI Dkt. Respicious Boniface wakati wa hafla ya utiaji saini mkataba huo
iliyofanyika kwa njia ya mtandao leo Jijini Dar es Salaam.
“ Mkataba huu wa Ushirikiano unamanufaa
makubwa upande wa gharama za vifaa tiba, kwani China ina viwanda vingi hivyo
itasaidia MOI kupata vifaa tiba kwa bei nafuu na kupelekea gharama za matibabu kushuka, ” Alisisitiza Dkt. Boniface
Akifafanua Dkt. Boniface amesema kuwa faida nyingine za mkataba huo ni kuimarisha ushirikiano baina ya MOI na CMA kwa kuwezesha wataalamu kutoka China kuja kutoa huduma nchini Tanzania na Wataalam wa Tanzania watapata fursa ya kwenda kujifunza nchini China.
Hafla
ya utiaji saini imefanyika kwa njia ya mtandao na kuhudhuriwa moja kwa moja
na Balozi wa Tanzania nchini China Mh.
Balozi Mbelwa Kairuki, Mkurugenzi Mtendaji wa MOI Dkt. Respicious Boniface
pamoja na wajumbe wa menejimenti ya MOI.
Kwa
upande wake, Balozi wa Tanzania nchini China Mhe. Balozi Mbelwa Kairuki amesema hatua ya Taasisi
ya MOI kuingia mkataba na Chama cha
Madaktari China (CMA) pamoja na hospitali ya Tian Tan italeta mapinduzi makubwa
kwenye utoaji wa huduma za kibingwa za mifupa, ubongo, mgongo na mishipa ya
fahamu hapa nchini Tanzania.
Taasisi ya Tiba ya Mifupa Muhimbili (MOI) imesaini mkataba wa ushirikiano na Chama cha Madaktari China (CMA) pamoja na hospitali ya Tian Tan kwa lengo la kuboresha huduma za kibingwa hapa nchini ikiwa ni moja ya hatua zinazochukuliwa na Serikali kupitia MOI.
Mkurugenzi Mtendaji wa MOI Dkt Respicious Boniface akiwasilisha mada wakati wa hafla ya utiaji saini kati ya MOI na chama cha Madaktari China (CMA).
. Balozi wa Tanzania nchini China Balozi Mbelwa Kairuki akiwa pamoja na viongozi wa Chama cha madaktari China (CMA) leo wakati wa utiaji saini kati ya MOI na chama hicho.(Picha zote na MOI)
Wajumbe wa Menejimenti ya MOI wakishuhudia hafla ya utiaji saini baina ya MOI na Chama cha Madaktari China (CMA) ili kuboresha huduma za kibingwa za Mifupa , Ubongo, Mgongo na Mishipa ya fahamu hapa nchini.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...