Na Pamela Mollel,Tarangire
Brenden Simonson, Mzungu mwenye asili ya Marekani, ana uwezo wa kuwasiliana, kuzungumza na kuelewana na wanyamapori aina ya Tembo
“Mimi huwa nazungumza na Tembo na wao wananielewa, wanaijua na sauti yangu. Hata nikiwakuta mbali porini naweza kuwatambua kwa majina niliyowapa na wao hunifahamu pia. Nikiwaita wanakuja hadi lilipo gari langu,” anaeleza Brenden.
Akiwa na umri wa miaka 29 tu, Brenden anasema ameweza kufahamiana vizuri na tembo kwa sababu yeye binafsi alizaliwa katikati ya pori, ndani ya hifadhi ya Tarangire na kuishi kama Tarzan.
Kutokana na hali hiyo, Brenden aliyezaliwa mwaka 1992, Tarangire ni moja ya matukio adimu ndani ya kipindi cha miaka 60 ya Uhuru.
“Tangu mtoto ninaishi katikati ya wanyamapori. Siwaogopi na wao pia hawanidhuru, wengi tunaelewana lugha, lakini hasa hasa Tembo ambao huwa tunawasiliana kabisa,” aliongeza.
Brendan anasimulia kwamba akiwa mtoto kulikuwa na tembo mkubwa kuliko wote hifadhini aliyejulikana kama ‘Thor’ na huyu alikuwa kama kiongozi wa Tembo wote, hata jina hilo ‘Thor’ alipewa kutokana na ukubwa wake maana ni jina la Moja wa ‘Mungu’ wa Kigiriki.
Tembo huyo mkubwa alikuwa akifika nyumbani kwao pale Tarangire ambako baba yake Brenden, Marehemu Jon Simmonson, alikuwa akiendesha biashara ya hoteli ya kitalii.
Hoteli hiyo iitwayo Tarangire Safari Lodge, ilianzishwa mwaka 1985 na mwekezaji Jon Simmonson, Mmarekani mkazi wa Ilboru Arusha, ambaye yeye na familia yake waliiendesha hadi alipofariki mapema mwaka huu.
Kwa mujibu wa Brenden Tembo ni wanyama waharibifu wa miundombinu na kuna wakati huvunja mabomba na kuangusha matenki ya Maji porini, hasa katika kipindi cha kiangazi.
“Lakini mimi nikifika katika eneo husika na waambia ‘Acha’ huwa wanaacha na kuondoka,” alisema.
Zaidi ya kuzungumza na wanyama, Brenden pia ana uwezo wa kuongea lugha kadhaa za asili zikiwemo zike za Kimasai na Kiswahili.Brenden kwa sasa ni moja ya vivutio katika hifadhi ya Tarangire maana wageni wengi hufika kwa ajili ya kushuhudia akizungumza na wanyama.
Tarangire ni hifadhi inayojulikana zaidi kwa kuwa na makundi makubwa ya Tembo ambao wanamaumbo makubwa kupita tembo wa sehemu nyingine.Askari Mhifadhi Daraja la kwanza katika hifadhi ya Tarangire Ali Omar anasema kuwa Baba yake Brenden,Mzee Jon Simonson ni mwekezaji wa awali kabisa katika eneo Hilo
"Tarangire Safari ndiyo lodge ya kwanza kuanzishwa toka 1985"
Brenden
Simonson akizungumza na waandishi wa habari katika hifadhi ya Tarangire
kuhusu maajabu aliyonayo ya kuongea na Tembo na kuelewana kabisa
Kundi la Tembo ambao hufika hoteli kwa Brendan
Brenden akionyesha picha kwa waandishi wa habari enzi akiwa mdogo pamoja na baba yake
Askari Mhifadhi Daraja la kwanza katika hifadhi ya Tarangire Ali Omari akiongea na waandishi wa habari
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...