TUME ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) inaendelea na zoezi la utoaji wa Elimu ya mpiga kura kwa njia ya ana kwa ana kwa wakazi wa jimbo la Ngorongoro ikiwa ni maandalizi ya uchaguzi mdogo wa Mbunge jimbo la Ngorongoro.
Elimu hiyo inatolewa kwa kutembelea kaya, maeneo ya mikusanyiko. Lengo ni kuwezesha wapiga kura wa jimbo la Ngorongoro kupata taarifa sahihi na elimu kuhusu masuala mbalimbali ya uchaguzi ili waweza kuwa katika nafasi nzuri ya kushiriki michakato ya uchaguzi.
Tume ya Taifa ya Uchaguzi imepewa mamlaka ya kutoa Elimu ya Mpiga kura nchi nzima na kuratibu taasisi na asasi ambazo zinatakiwa kutoa Elimu hiyo kupitia kifungu ha 4C cha Sheria ya Taifa ya Uchaguzi, Sura 343.

Elimu ya mpiga kura imetolewa kwa wanafunzi wa shule ya Sekondari Sale iliyopo kata ya Sale , jimbo la Ngorongoro.



Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...