Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Mhandisi.Robert Gabriel, akizungumza na wafanyabiashara wadogo (machinga) katika Soko la Ukwaji, Igoma juzi.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Jiji la Mwanza, Seleman Sekiete akizungumza mbele ya machinga (hawapo pichani) kuhusu uboreshaji wa soko na utatuzi wa changamoto za soko la Ukwaju juzi.
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Mhandisi.Robert Gabriel, akisistiza jambo alizpofanya mkutano na machinga nje ya soko la Ukwaju juzi.Picha na Baltazar Mashaka



*************************

NA BALTAZAR MASHAKA,Mwanza


SERIKALI itaendelea kutoa kipaumbele cha mikopo isiyo na riba kwa wajasiriamali ili kuboresha biashara,mazingira na uwekezaji.

Mkuu wa Mkoa wa Mwanza,Mhandisi.Robert Gabriel,alisema jana wakati akizungumza na wafanyabiashara wa Soko la Ukwaju,katika Wilaya ya Nyamagana.

Serikali iko kwenye mchakato wa kuanzisha Saccos kwa ajili ya kuwakopesha machinga na kuwawezesha kuboresha biashara yao,mazingira ya biashara na uwekezaji.

“Bado mambo kadhaa yanafanyika na baada ya wiki chache tutafungua Machinga Saccos, kinachosubiriwa ni utaratibu.Tunawafahamu machinga wanaofanyabiashara hapa ili fedha hii tunayowakopesha isipotee lazima tuwahakiki tuwe na taarifa kibanda hiki anakimiliki nani apewe mkopo,”alisema Mhandisi.Gabriel.

Alisema neema imeingia na kuwataka machinga walioko mtaani,watoke huko waingie kwenye masoko waliyopangiwa wafanye biashara na kunufaika wa sababu serikali imedhamiria kuboresha maisha ya makundi yote.

Mkuu huyo wa mkoa alieleza kuwa fedha za mikopo ya asilimia 10 inayotolewa na halmashauri kwa wajasiriamali bila riba,itatolewa kwa mkakati kwa wanawake, walemavu na vijana wanaofanyabiashara kwenye masoko rasmi.

“Hatuwezi kusema tunawapanga halafu ana kuja mtu anachukua maeneo kwa majina tofauti,haki na kweli lazima visimame na machinga waheshimiwe,”alisema Mhandisi.Gabriel.

Alishauri utaratibu ufanyike, uundwe uongozi unaoeleweka na kuonya kama kuna mtu kajichukulia vibanda kwa majina tofauti wakiwemo watakaoshindwa kufungua biashara ndani ya wiki mbili watapokonywa na kupewa watu wengine.

Mhadisi.Gabriel alisistiza machinga wasipoteze fursa ya kupata mikopo isiyo na riba, hivyo wapewe elimu wapate mikopo hadi waikimbie lakini wakumbuke kurejesha.

Mkurugenzi wa Jiji la Mwanza, Seleman Sekiete,alisema elimu itaanza kutolewa kabla ya machinga kupata mikopo hiyo isiyo na riba lakini ipo changamoto ya baadhi ya machinga kurudi kupanga bidhaa na kufanya biashara kwenye maeneo yasiyo rasmi walikoondolewa kutokana na wafanyabiashara wakubwa kutoa bidhaa kwa wafanyabiashara hao wadogo.

Pia yameibuka masoko holela kwenye baadhi ya vichochoro na baadhi ya stoo zimegeuka maduka,hivyo watahakikisha yanadhibitiwa ili kuwapa nguvu machinga waliotii na kuhamia kwenye masoko mapya.
“Changamoto ya machinga kurudi walikoondolewa hatua zinachukuliwa, wanaokaidi wanatozwa faini,tuntaka wakafanye biashara,waende walikopangiwa wateja watakuja kupata huduma huko,”alisema Sekiete na kusistiza kuwa serikali itaendelea kuyaboresha masoko hayo yawe na hadhi ya kimataifa.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...