Washiriki wa kongamano hilo wakiimba wimbo uliokuwa na maishairi yanayosema Rais Samia tutamlinda na kumtetea.Wimbo huo ulikuwa ukiimbwa wakati wa kongamano hilo baada ya mmoja ya washiriki alipoamua kusimama na kuwaomba waimbe wimbo huo.




Na Said Mwishehe, Michuzi TV

MKURUGENZI na Mwanzilishi wa Taasisi ya Purple Planet Hilda Kasoka amesema huu ni wakati makundi yote katika jamii likiwemo la wanawake kuhakikisha wanamuunga mkono Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan katika malengo yake ya kuwawezesha wanawake kiuchumi kupitia majukwaa mbalimbali.

Ameyasema hayo katika ukumbi wa Mliman City jijini Dar es Salaam ambapo kumefanyika Kongamano la wanawake mwaka 2021 lililoandaliwa na Purple Planet na kushirikisha wadau wengine wa maendeleo ambapo lengo lao ni kumuinua kiuchumi mwanamke ,mtoto wa kike nchini Tanzania.

"Leo tumekutana Mliman City kufanya kongamano la mwaka pamoja na kuzindua programu ya Women in Action ambayo tunakwenda nayo mwaka 2022,Programu hiyo inahusu kuwajenga na kuwasaidia wanawake katika masuala ya uwezeshaji na uwekezaji zaidi ,tumetoa sana elimu toka mwaka 2017 tumefikia wanawake zaidi ya 10,000 na baadhi yao wamehitimu mafunzo hapa leo.

"Sasa ni wakati wa kumuunga mkono Rais Samia Suluhu Hassan kupitia programu mbalimbali ambazo tunazifanya kama taasisi binafsi lakini tutashirikiana na Serikali kupitia Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi ambao ni wadau wetu.Tunamshukuru Naibu Waziri wa Maji Mary Prisca Mahundi ambaye amekuwa mgeni rasmi ,amefungua programu hii na huu ni uzinduzi tu.

"Utekelezaji unakwenda kufanywa sio tu na Purple Planet ,bali kutakuwa na taasisi mbalimbali ambazo tumeshirikiana hapa leo, tutakuwa na taasisi viwanja, Vicoba, benki ambazo zitakwenda kusaidia kutoa mitaji kwa wanawake maana lazima watu wawe na fedha,"amesema.

Ameongeza kutakuwa na watu ambao watakuwa wanatoa elimu mbalimbali, kwa hiyo wanakwenda kushirikiana kuhakikisha wanamuunga mkono Rais Samia kwenye mambo mbalimbali ya uwezeshaji hasa nia yake ya kuwezesha wanawake kiuchumi na kutoa fursa za kiuchumi kwa siku za usoni.

Kuhusu mikoa ambayo programu hiyo itaanzia ni Dar es Salaam na Pwani ,Kanda ya Kaskazini ,Kanda ya Ziwa,Kanda ya Kati kwa maana ya Dodoma na Singida ,pia watakwenda Zanzibar kwa ajili ya kushirikiana katika kuwawezesha wanawake kiuchumi kule Zanzibar.

"Programu ambayo tumeizindua inakwenda kusaidia moja kwa moja wanawake 1000 kwa kuhakikisha tunawatengeneza waweze kusimama katika biashara na shughuli za kiuchumi wanazofanya,kubwa waweze kurasimisha biashara watambulike ,waongeze mitaji yao na kutumika kama chachu kwa wale wengine ambao wanakuwa wanaanza chini.

"Tunajua nia ya Rais ya kuwezesha wanawake kiuchumi kupitia jukwaa la taifa la uwezeshaji wanawake ,hivyo kupitia wanawake ambao wako hapa leo, kupitia wanawake 1000 wanaokwenda kufikiwa moja kwa moja na programu tuliyoizindua ambao watakuwa wanufaika watakuwa chachu katika majukwaa mbalimbali ya kiuchumi na kijamii, na ndio maana halisi ya Women Action in Tanzania,"amesisitiza .

Ametoa mwito kwa wanawake wote waweke tofauti zao kando, waungane kwa pamoja kufanya ajenda ya mwanamke kuwa ajenda ya kitaifa."Tumuunge mheshimiwa Rais mkono kama ambavyo tumeimba leo tutamlinda na kumtetea ,twende tukamtetee kwa shughuli zetu , kila mtu akawe Samia katika eneo lake,hii ndio njia nzuri ya kumlinda Rais wetu".

Alipoulizwa je adui wa mwanamke ni mwanamke, amejibu adui wa mwanamke ni umasiki,magonjwa ,udhaifu wake.Hivyo wanawake wachape kazi kwa bidii na wamuunge mkono Rais Samia ambaye ametoa katika uongozi kwa kufika nafasi ya juu kabisa katika nchi.

"Tunakwenda kuelekea 2025 na 2030 tutafanya tathimini,tunajua kuna wanaume wengi ambao wanatuunga mkono kwenye hii, ajenda ya kumuwezesha mwanamke tumesema ni ya kitaifa , sio ajenda ya kike ila imeanzishwa tu na wanawake,kwa hiyo makundi yote watuunge mkono kuhakikisha tunawasaidia wanawake kupata uhuru wa kiuchumi na haki za kiuchumi".

Kwa upande wake mgeni rasmi katika kongamano hilo Mary Prisca Mahundi ambaye ni Naibu Waziri wa Maji pamoja na mambo mengine amempongeza Hilda Kisoka kwa juhudi anazofanya za kuwaunganisha wanawake na kuwa daraja la kuwawezesha kiuchumi kupitia programu mbalimbali huku akiwataka wanawake wote nchini kuwa kitu kimoja na kutumia majukwaa yaliyopo kushiriki katika maendeleo.

Amewakumbusha kuchangamkia mikopo inayotolewa na Serikali kupitia halmashauri huku akitumia nafasi hiyo kuelezea mikakati iliyowekwa na Rais Samia Suluhu Hassan katika kuboresha maisha ya wananchi wakiwemo wanawake.
Naibu Waziri wa Maji Mary Prisca Mahundi( wa sita kushoto) akiwa na wageni wengine waalikwa wakishuhudia uzinduzi wa programu ya Women in Action ambayo inalenga kuwainua na kuwawezesha wanawake kiuchumi.Programu hiyo imeandaliwa na Taasisi ya Purple Planet.
Naibu Waziri wa Maji Mary Prisca Mahundi akizungumza wakati wa kongamano la wanawake mwaka 2021 lililoandaliwa na Purple Planet sambamba na kuzindua programu ya Women in Action.
Mkurugenzi na Mwanzilishi wa Purple Planet akizungumza wakati wa kongamano hilo ambapo ametoa rai kwa Watanzania hasa wanawake kumuunga mkono Rais Samia katika jitihada zake za kuleta maendeleo.


Naibu Waziri wa Maji Mary Prisca Mahundi akizungumza wakati wa kongamano la wanawake mwaka 2021 lililoandaliwa na Purple Planet sambamba na kuzindua programu ya Women in Action.
Katibu Mkuu wa Baraza la Taifa Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi Beng'i Issa akizungumza wakati wa kongamano hilo lililofanyika Mliman City ,Dar es Salaam na kuhudhuria na wadau wa maendeleo kutoka taasisi mbalimbali


Naibu Waziri wa Maji Mary Prisca Mahundi( wa sita kushoto) akiwa na wageni wengine waalikwa wakishuhudia uzinduzi wa programu ya Women in Action ambayo inalenga kuwainua na kuwawezesha wanawake kiuchumi.Programu hiyo imeandaliwa na Taasisi ya Purple Planet.
Baadhi ya washiriki wakifuatilia majadiliano wakati wa kongamano hilo ambalo lilihudhuriwa na watu wa kada mbalimbali.


Matukio mbalimbali katika picha wakati wa kongamano hilo lililokwenda sambamba na uzinduzi wa Program ya Women in Action.





Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...