Na Pamela Mollel,Karatu

Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania,Samia Suluhu amemwaga Neema Kwa wakazi wa Karatu Kwa kuwapatia sh 10.5 bilioni na kuwajengea Daraja 

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Utawala Bora, Mohamed Mchengerwa akizungumza, wakati kamati ya kudumu ya Bunge ya Utawala bora na Serikali ya Mitaa, ilipotembelea kijiji cha Laja kuzindua darasaja lililojengwa na TASAF na wananchi kuomba kujengewa daraja jingine ili kuondoa adha ya kukwama kufika eneo la Eyasi amesema Rais amesikia kilio chao .

Mchengerwa amesema Rais Samia Suluhu anataka kuona maisha ya watanzania yanabadilika hivyo licha ya kutolewa sh 10.5 bilioni na Kupitia TASAF Sasa amekubali kuwajengea daraja Wananchi wa Karatu.

"nimeongea na Rais Samia Suluhu amekubali atajenga daraja kuunganisha Laja na Eyasi kama ambavyo mmeomba na naagiza TASAF kuanza kufanya tathimini kushughulikia suala hili "amesema

Awali Mwenyekiti wakamati ya kudumu ya bunge ya Utawala na Serikali za mitaa, Abdalah Chaurembo, alisema serikali kero za Wananchi wa Karatu zitafanyiwa kazi.

Aliwataka viongozi waKaratu, kushirikiana na Wananchi kubuni miradi ambayo itakwenda kutatua kero zao.

Awali Mbunge wa Karatu, Daniel Awakie amesema, wilaya yaKaratu inakabiliwa na changamoto nyingi, ikiwepo tatizo la uhaba wa miundombinu na hivyo akaomba serikali kusaidia kutatua kero.

Alisema anashukuru serikali Kwa kuendelea kutoa fedha kusaidia miradi katika wilaya hiyo nakuomba isichoke kwani wilaya bado ipo nyuma.
Wabunge wa Kamati ya kudumu ya Bunge ya Utawala Bora na serikali za mitaa wakizindua daraja lililojengwa na TASAF katika Kijiji cha  Laja Wilayani Karatu
Picha ikionesha Lori likipita juu ya daraja mara baada ya kamati ya kudumu ya Bunge Utawala na serikali za mitaa ilipozindua daraja hilo lililojengwa na TASAF katika Kijiji cha laja wilayani Karatu
Waziri wa nchi ofisi ya Rais Utawala Bora Mohammed Mchengerwa akizungumza na wananchi wa kijiji cha laja wilayani Karatu mara baada ya kamati ya kudumu ya Bunge Utawala na serikali za mitaa ilipofika kuzindua daraja hilo
Wananchi wakifatilia uzinduzi wa daraja

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...