Na Pamela Mollel, Monduli

Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Mh.Samia Suluhu Hassan ametunuku kamisheni kwa maafisa wanafunzi katika chuo Cha mafunzo ya kijeshi Monduli mkoani Arusha


Maafisa hao wapya ni kundi la 02/18-Shahada ya Sayansi ya kijeshi (BMS)idadi 61 ambao wamepata mafunzo miaka mitatu na kuhitimu shahada ya Sayansi ya kijeshi pamoja na kundi la 08/18 Jeshi la Anga idadi 56 waliopata mafunzo katika shule ya Anga ya kijeshi hapa Nchini


Aidha katika wahitmu hao kuna marubani wa ndegevita,Marubani na Wahandisi Ndege  huku waliopata kamisheni jumla yao ni 118,kati yao wanaume 99 na wanawake 19


Zoezi la kutunuku kamisheni kwa maafisa hao lilifanyika kwa mara ya kwanza na Rais na Amir Jeshi Mkuu tangu alipoapishwa kuwa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu na ni mara ya pili kutunuku kamisheni ambapo mara ya kwanza ilikuwa tarehe 17 April 2021 Ikulu jijini Dodoma


Kabla ya kutunuku kamisheni,Rais Mama Samia amekagua Gwaride lililoandaliwa na maafisa wanafunzi hao na baadae aligawa zawadi kwa wanafunzi waliofanya vizuri zaidi kwa kila kundi


Wakati huo huo  Rais Mama Samia alitunuku shahada ya kwanza ya Sayansi ya kijeshi kwa maafisa wapya 61


Mafunzo ya shahada hiyo yaliendeshwa katika chuo Cha  mafunzo ya kijeshi Monduli kwa kushirikiana na chuo cha Uhasibu njiro (IAA)


Sherehe hizo zilihudhuliwa na viongozi mbalimbali wakiwepo wakuu wa vyombo vya ulinzi na usalama ,wawakilishi wa nchi rafiki ,makamanda,walezi na wawazi wa maafisa wapya

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...