Na Khadija Kalili, Pwani
Mkuu wa Mkoa wa Pwani Alhaj Abubakari Kunenge ameamuru kuchukuliwa hatua za kinidhamu kwa Mtendaji wa Kata ya Mtambani Wilayani Kibaha kwa kushindwa kudhibiti wakulima wa mbogamboga kwenye kitongoji cha Kwa Dosa ambao wanavuta maji kutoka chanzo cha mto Ruvu.
RC Kunenge amezuia matumizi ya umwagiliaji na unyweshaji wa mifugo kwa watu wanaotumia vyanzo vya mito ili kukabiliana na upungufu wa maji kwenye mito ndani ya mkoa huo.
Alhaji Kunenge ameyasema hayo leo alipotembelea kuangalia shughuli zinazofanywa kwenye vyanzo vya maji vya mto Ruvu eneo la Dosa na Kidogozero ambapo kuna baadhi ya watu wanajishughulisha na kilimo na unyweshaji mifugo kunakosababisha uhaba mkubwa wa maji kwenye Mkoa wa Pwani na Dar es Salaam
Awali Afisa wa Bonde la mto wami Ruvu Halima Faraji amesema wamefanya hivi karibuni opereshen Kwenye maeneo hayo na kubaini wapo watumiaji wengi wa maji wasio rasmi pamoja na mifugo
Pia amesema watumiaji maji 300 ndio wenye vibali wanaotambulika pekee.
Afisa huyo ameongeza kuwa, kwa data za novemba 15 walipofanya ukaguzi walikuta maji Lita 4100 yalikuwa yanapita mtano humo kwa sekunde na Sasa yameongezeka kwa sababu data za Jana novemba 18 wamekuta Lita 6430 ndio zinapita kwa sekunde hivyo Kuna ongezekoa linaonekana maji yanaongezeka
RC Kunenge ametoa agizo hilo leo alipotembelea bonde la mto Ruvu akiwa na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa na ya Wilaya za Kibaha,Kisarawe, na Bagamoyo .
"Kuanzia leo Novemba 19 hakuna ruhusa mtu yeyote kufanya shughuli za umwagiliaji,kilimo wala kunyweshewa mifugo hadi hapo serikali itakapotoa maelekezo mengine.
"Kamati ya Ulinzi na Usalama Mkoa na Wilaya tatu za Kibaha, Bagamoyo na Kisarawe tumekuja kufanya ukaguzi wa eneo la bonde la mto Ruvu ukiwa niutekelezaji wa agizo la Rais Samia Suluhu Hassan alivyoelekeza shughuli za kilimo na umwagiliaji kwenye maeneo ya vyanzo vya maji visimame kwanza kwani wakati huu kuna uhaba wa maji " alisema RC Kunenge.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...