Na Khadija Seif, Michuzi Tv
WANAWAKE wajasiriamali kupitia jumuiya ya Rich Women Forever wanatarajia kuibuka na mpango mkakati wa kusaidia wanawake wanaotaka kuingia na walio kwenye biashara ili kufuta dhana ya ugolikipa katika familia zao
Akizungumza na Michuzi Tv,Muasisi wa Jumuiya ya Rich Woman Forever Amina Ntomola amesema wamejiita 'Rich Woman Forever' kama chachu kwa mwanamke yeyote mwenye ndoto za kutimiza malengo mbalimbali ya kimafanikio ili kuendana na dhamira waliyokusudia ya Kusaidia wanawake wengine.
"Tumezindua rasmi jumuiya yetu ya Rich Woman Forever ndani yake kutakua na majukwaa ambayo yatatoa elimu ikiwemo elimu ya afya,biashara, Uhusiano pamoja mengine mengi lengo likiwa ni kwa namna gani tutawapa njia sahihi wanawake Kuanza biashara wanazozihitaji na kufuta dhana iliyojengeka katika jamii kuwa Wanawake wengi ni golikipa".
Ntomole ameongeza kuwa wamelenga kuwapa elimu wanawake wote na mbinu za kufanikiwa katika biashara, afya na mahusiano wakiamini kwa kufanya hivyo kutamuwezesha mwanamke kufanikiwa.
Pia ameeleza tukio hilo limeanza kwa kuwahusisha wanawake wa mikoa ya Dar es Salaam, Morogoro na Pwani na zaidi limelenga kumfanya mwanamke kuwa shujaa katika dhamira yake.
"Kupitia umoja huu tunataka kuisadia jamii katika nyanja mbalimbali ili waondokane na changamoto i za kimaisha na hivyo kusaidia kutimiza ndoto zao.Kuanzishwa kwa umoja huo ni fursa kwa jamii hususani ya wanawake kufanikiwa kimaisha.
"Na hivyo kutimiza malengo yao ya kimaisha sambamba na kuwezesha maendeleo ya Taifa kwa ujumla kwani tuna mikakati ya kurudisha kwa jamii ikiwemo kuchangia vifaa shuleni,taulo za kike na vitu mbalimbali ambavyo jamii inahitaji sana,"amesema.
Muasisi wa Kikundi cha Wanawake wajasiriamali "Rich Women Forever" Amina Ntomole akizungumza kwa namna gani wataweza kuwafikia kufuta dhana ya wanawake tegemezi yani "golikipa" pamoja na kwa jinsi gani Elimu ya Afya, Mahusiano itatolewa kwa wanawake watakaoanza kuingia kwenye ujasiriamali kwa lengo la kujikwamua kiuchumi na kusaidia familia zao
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...