Na Anneth Kagenda
TAASISI ya Liwancy Nchini Tanzania inayojishughulisha na Kilimo cha mazao mbalimbali kubwa likiwa ni zao la korosho imekutana na wadau pamoja na waandishi wa habari lengo likiwa ni kumpongeza mama Samia Suluhu Hassan kwa utekelezaji wake wa kazi iliyotukuka.

Kadharika, Mshauri wa Liwancy Nchini Charles Sabinian (Lowassa), ambaye pia ni Kada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), amempongeza kwa dhati utendaji wa Rais Mama Samia na kusema kuwa awali alizulu Bagamoyo na kutembele, ngome ya Kaole na kujionea mambo mbalimbali na kusema kuwa mwanamke alitabiliwa kwamba ataongaza miaka ijayo.

"Na kwa sasa utabili huu umedhihirika kwamba Mama Samia ndiye anayeongoza Nchi kwa sasa."

Lowassa, kwenye kikao hicho amesema kuwa mama Samia amekuwa msaada mkubwa kwa vijana kwani hata machinga amewatafutia maeneo ya kufanya shughuli zao.

Aidha, amesema kuwa Rais pia amekua mstari wa mbele kuwatete vijana wa kitanzania kuwatetea vijana wa kitanzania katika kuhakikisha wanajipatia kipato kutokana na kwamba anaenzi uongozi wa Hayati Magufuli.

Mshauri wa Liwancy Lowassa, amesema kuwa Rais Samia amekuwa akifanya mambo makubwa ambayo hata kwa vijana yamekuwa yakileta tija kwa nchi.

Mwakilishi wa Liwancy ambaye ni Msaidizi wa CEO George Solo, amesema kuwa mkutano wa jana ulikuwa kwa ajili ya kukutana na waandishi wa habari pamoja na wadau wa maendeleo ili kujadili maendeleo ya kampuni.

George, amesema kuwa lengo pia lilikuwa kumpongeza Mama Samia kwa utendaji wake wa kazi kubwa na uliotukuka ikiwemo kufuatilia mambo ya maendeleo ya vijana wa nchi yake.

Hata hivyo amesema kuwa wanampango wa kuajili vijana wengi zaidi kwenye Taasisi yake ili kuepukana na tatizo la umaskini nchini.

Mgeni mwalikwa Kijana Kiboko Manyerere Nyerere, alisema kuwa kikao hicho ni cha msingi na kwamba wanaiomba serikali kuunga mkono taasisi ya Liwancy kwani iko kwa ajili ya kuwasaidia vijana na kumuunga mkono mama.

Manyerere amewaomba vijana kuchangamkia fursa na kuendelea kumuunga mkono mama Samia katika utekelezaji wa majukumu mbalimbali ya Nchi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...