KAMPUNI  ya TotalEnergies Marketing Tanzania Limited ambayo awali ilijulikana kama Total Tanzania Limited imezindua wiki ya huduma kwa wateja ya TotalEnergies kwa mwaka 2021, yenye kaulimbiu ya 'Tujenge kesho pamoja.'

Hii ni awamu ya tatu ya wiki ya huduma kwa mteja ya TotalEnergies tangu ianzishwe mwaka 2019. TotalEnergies inaendelea kuonyesha dhamira yake kwa Tanzania kwa kuwakaribisha wateja wao ili kushiriki maono yao ya mustakabali wa kampuni ya TotalEnergies Marketing Tanzania Limited nchini. 

Akizungumza wakati wa hafla hiyo, Mkurugenzi Mkuu wa kampuni, Jean-Francois Schoepp amesema kuwa ni muhimu wananchi washirikishwe katika mnyororo huo wa utoaji huduma.

''Kama baba wa Taifa, Hayati Mwalimu Julius Nyerere aliwahi kusema kuwa, Ikiwa maendeleo ya kweli yatatokea, ni lazima wananchi washirikishwe Pia tunaamini kwamba TotalEnergies Marketing Tanzania Limited itaendelea kukuwa zaidi endapo tutawashirikisha wateja wetu wateja wetu na kuwa tayari kukidhi mahitaji kikamilifu.” Amesema.

Schoepp amewashukuru wateja wao kwa kuendelea kuwaamini kutoka enzi za Total hadi kufikia mabadiliko yao ya ya TotalEnergies na kuahidi kuendelea kutoa huduma bora zenye viwango vya hali ya juu.

Wafanyakazi wa TotalEnergies Marketing Tanzania Limited wakiongozwa na mkurugenzi mkuu, Bw. Jean-Francois Schoepp wametoa huduma kwa wateja waliotembelea kituo cha TotalEnergies East Oysterbay siku ya Jumatatu na kupata fursa ya kusikiliza maoni ya wateja, kuboresha mahusiano na wateja wao kwa nia ya kuziba mapengo yoyote yaliwepo na kuweza kujenga TotalEnergies Marketing Tanzania Limited kwa pamoja na wateja wao.

Zaidi ya hayo, wateja walipata nafasi ya kucheza gurudumu la bahati katika kituo hicho na walijishindia zawadi kadhaa zikiwemo fulana, chupa za maji, kofia, bidhaa za kutunza magari kama vile baridi na air freshener, na vocha ya zawadi zilizowawezesha kununua bidhaa zozote katika duka la Cafe Bonjour lilipo kituoni hapo.

TotalEnergies Marketing Tanzania Limited imekuja na taswira mpya na kuwa
 wabunifu zaidi, hii inaakisiwa kikamilifu na ushirikishwaji wa wateja wao kwa nia ya kuboresha ubora wa bidhaa na huduma zao ili kukidhi kila Mtanzania anayehitaji huduma za mafuta, vilainishi, pamoja na bidha zipatikanazo madukani.











Matukio mbalimbali katika uzinduzi wa awamu ya tatu ya huduma kwa wateja ya TotalEnergies.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...