WAKALA  wa Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) umeendesha semina elekezi ya kuwajengea uwezo na kutoa elimu kwa viongozi wa Wilaya ya Ubungo mkoani Dar es Salaam kwa Madiwani na Wawakilishi wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama.

Semina hiyo ilijikita katika kufafanua kwa kina  kuhusu mfumo mpya wa Kielektroniki wa malipo ya Ushuru wa maegesho ya magari ambao unatarajia kuanza Desemba 1,2021.

Akifungua semina Mkuu wa Wilaya ya Ubungo, Kheri James ameipongeza TARURA kwa kuandaa semina hiyo na amehaidi kutoa ushirikiano.Ofisi ya Rais ya Rais TAMISEMI, TARURA kwa kushirikiana na Wizara ya Fedha na Mipango wameboresha mfumo, sasa kumbukumbu namba (Control number) itapatikana ndani ya dakika moja kwa kutumia njia ya kutolewa ankara kupitia kwa Mkusanya Ushuru 

 Kwa kutumia TeRMIS App (inayopatikana PlayStore), Kwa kutumia GePG App (inayopatikana PlayStore & AppStore), Kwa kutumia simu ya mkononi Piga *152*00# kisha fuata maelekezo na Kwa kutumia Wavuti ya mfumo inayopatikana kwa www.termis.tarura.go.tz.

Pia, TARURA imeboresha eneo la utoaji wa Elimu kwa kuanzisha Dawati la Malalamiko na kuweka namba za simu ambazo ni 0733-149658, 0733–149659 au 0733-149660 na kupitia namba hizi mteja atapiga simu na kutatuliwa changamoto yake. Pia anaweza kuwasilisha lalamiko lake katika Ofisi za TARURA zilizopo karibu yake.

Katika semina hiyo washiriki wa semina hiyo wameelezwa jinsi ambavyo unatakiwa kulipa maegesho kidigitali ambapo mhusika atatakiwa  kutumia simu ya mkononi

Piga *152*00#

1. Chagua 4 (Nishati, Madini na Usafiri)

2. Chagua 2 (TARURA)

3. Chagua 1 - Lipia Maegesho

4. Ingiza namba ya chombo cha Moto

5. Utapokea ujumbe mfupi

6. Bonyeza 1 Kuendelea

7. Ingiza namba ya Siri

8. Bonyeza 1 Kuthibitisha malipo ya Serikali.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...