Mtalaam wa masuala ya Mtandao Dotto Mnyadi akifafanua jambo wakati wa kikao kazi kilichoandaliwa na DCEA kwa waandishi wa habari za kidigitali.
 

Na Said Mwishehe, Michuzi TV

WAANDISHI wa habari za kidigitali kutoka vyombo mbalimbali vya mtandaoni wamepiga kambi mkoani Morogoro kwa ajili yamafunzo ya kujengewa uwezo wa kuandika habari zinazohusu dawa za kulevya .

Kwa mujibu wa waandaji wa mafunzo hayo ambao ni Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya( DCEA) imeona haja ya kuwakutanisha waandishi hao hasa wanaoandika habari katika mitandao ya kijamii katika kuandika na kuripoti.

Mada mbalimbali zimetolewa na watalaamu wa DCEA na hivyo kuwafanya waandishi kuelewa mengi ambayo hawakuwa wanayafahamu kuhusu madhara yanayotokana na utumiaji wa dawa za kulevya, kinga na jinsi ya kuzuia jamii kutoingia katika kutumia dawa hizo 

Mbali ya waandishi hao walioko katika mafunzo kukaa darasani( ukumbi wa mkutano) pia wamepata nafasi ya kusikiliza shuhuda zilizokuwa zinatolewa na baadhi ya vijana waliokuwa wanatumia na sasa wameamua kuacha kutumia dawa za kulevya kwa hiyari yao na wamekuwa mabalozi wa kuelezea madhara yanayotokana na utumiaji wa dawa hizo.

Pamoja na kusikia shuhuda hizo waandishi hao kutoka vyombo 30, wamepata nafasi ya kutembelea Sober House ya Free at Last iliyopo Kihonda mkoani Morogoro na wakiwa wapo wameshuhudia namna ambavyo waraibu wa dawa hizo wanavyoishi na jinsi wanavyopata matibabu.

Katika mafunzo hayo DCEA imeona haja ya kuwakutanisha waandishi hao na Mtalaam mbobezi wa masuala ya habari za mitandao ambaye alitumia nafasi yake kueleza kwa kina jinsj ambavyo waandishi wanaweza kuandika habari, kuripoti na kutangaza na jami ikapata elimu sahihi kuhusu masuala yanayohusu dawa za kulevya.










Matukio mbalimbali katika picha wakati wa kikao kazi cha waandishi wa habari za kidigital kilichoandaliwa na Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya mkoani Morogoro.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...