UTOAJI wa takwimu za masuala mbalimbali yanayotokea nchini ikiwemo taarifa za UVIKO-19 na masuala ya kijinsia yameonekana kuwa kikwazo hali iliyopelekea Tanzania kushindwa kufanya vizuri katika makubaliano na mikataba iliyosainiwa na Serikali kidunia na kikanda kuhusiana na masuala ya kijinsia (Gender Barometer 2021.) ambayo pia yameorodheshwa na kusukumwa katika utekelezaji na Umoja wa nchi za kusini mwa Afrika (SADC,) na kupimwa kupitia 'SADC Gender Protocol."

Masuala yaliyoikwamisha Tanzania ni pamoja na upatikanaji wa data hasa za visa na vifo vitokanavyo na UVIKO-19, mimba za utotoni, utekelezaji mdogo wa haki za afya ya uzazi na ukatili wa kijinsia yameikwamisha Tanzania kushindwa kufanya vizuri katika kipimo cha SADC Gender Barometer ya mwaka 2021.

Mtandao wa Jinsia (TGNP,) chini ya mwavuli wa Mtandao wa Kusini mwa Afrika (Southern Africa Gender Protocol Alliance) ulikutana na asasi za kiraia za 'Women Right Organization' (WRO's) arobaini zinazoongozwa na vijana na zinazoangalia masuala ya kijinsia hasa katika masuala ya mazingira, afya ya uzazi na masuala ya ndoa za utotoni huku sababu za kuchaguliwa kwa kundi hilo zikielezwa ni kutokana na Tanzania kutofanya vizuri katika maeneo wanayoyashughulikia.

WRO's zilikutana na kuzindua wasilisho hilo na kujadili ni kwa namna gani Tanzania inaweza kuendana na utekelezaji wa SADC Gender Protocal na kuweka mkakati wa kusaidia Serikali na jamii katika utekelezaji wa SADC Gender Protocal katika makubaliano ambayo nchi ilisaini kwa uboreshaji zaidi.

Akiwasilisha mada katika warsha hiyo Msimamizi wa Idara ya utetezi na Ujenzi wa Nguvu za Pamoja kutoka Mtandao wa Jinsia (TGNP,) Joyce Mkina alifafanua namna utoaji wa takwimu za UVIKO-19 ulivyominywa kwa mujibu kwa kipimo cha 'Gender Barometer 2021'

Bi. Mkina alieleza kuwa takwimu zinaonesha kuwa takwimu za UVIKO-19 nchini zilichukuwa takribani mwaka mmoja au miwili hadi kutolewa kwake, kutokuwa na takwimu za UVIKO-19 hadi kufikia Agosti mwaka huu licha ya madhara ya mlipuko wa virusi hivyo kuonekana wazi.

Kwa mujibu wa SADC Gender Barometer 2021 hakuna takwimu zinazoonesha idadi ya visa vya UVIKO-19 na vifo kwa wanawake na wanaume licha ya madhara kuonekana.

Kuhusiana na masuala ya kijinsia ikiwemo masuala ya afya ya uzazi ikiwemo hedhi salama bado kumekuwa na changamoto ya kodi kwa taulo za kike pamoja wanafunzi kutopata taulo hizo bure mashuleni.

Changamoto nyingine zilizobainika katika ripoti ya Gender Barometer ni pamoja na kuongezeka kwa mimba za utotoni, asilimia 31 ya mabinti kuolewa kabla ya kufikia umri wa miaka 18, kuongezeka kwa vitendo vya unyanyasaji wa kijinsia kwa asilimia 20 hasa wakati wa mlipuko wa virusi vya UVIKO-19 (Lockdown.)

Katika masuala ya uongozi hasa nafasi za uwakilishi wa wanawake Tanzania imefanya vizuri kwa kupanda kwa asilimia 37 kutoka asilimia 29 mwaka 2009 pamoja na eneo la utoaji wa elimu kuhusu UKIMWI Tanzania imeonekana ikifanya vizuri kwa mujibu wa ripoti hiyo.

Mkutano huo wa mwaka ulilenga kujadili namna bora ya kujadiliana na Serikali katika utekelezaji wa mikataba ya kijinsia ambayo Serikali imesaini kikanda na kidunia ambayo pia SADC imeyaorodhesha na kuweka nguvu katika utekelezaji wake kupitia 'SADC Gender Protocol.'

Asasi zilzoshiriki kikao hicho ni pamoja na Salha Foundation, SAWA, YUNA, UMATI, Binti Makini, Msichana Initiative, Mwanamke na Uongozi, Mtandaao wa jinsia na vyombo vya habari, KC Saranga, Malala Fund, na Iccao ambazo kwa kiasi kikubwa zinashughulika na masuala ya jinsia na hasa kwa kundi la wanawake.





















































































Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...