Wafanyabiashara maarufu nchini Oman wanatarajiwa kufanya ziara nchini tarehe 25 Novemba 2025 kwa ajili ya kukamilisha taratibu za kupata eneo mkoani Tanga la kukusanyia mifugo hai ya kusafirisha Oman kupitia bandari ya Tanga.

Wafanyabiashara hao ambao ni Mkurugenzi Mwendeshaji wa Abu Suleiman Al-Darai Trading &Services, Bw.  Mohamed S. Aldarai; Afisa Mtendaji Mkuu wa Desert Cold Store LLC, Dkt. Munawar H. Pardhan; Mkurugenzi wa Desert Cold Store LLC, Bw. Aasim M. Pardhan na Mkurugenzi wa IKTIMAl Trading Company LLC, Bw. Salem Al Dighaishi awali walikuwa wanasafirisha nyama iliyogandishwa tani 240 kwa mwezi kutoka nchini walifanya mazungumzo na Balozi wa Tanzania nchini Oman, Mhe. Abdallah Kilima hivi karibuni kuhusu taratibu za utekelezaji wa biashara yao hiyo.

Mhe. Balozi aliwapongeza wafanyabiashara hao kwa kuonesha nia ya kufanya biashara na Tanzania kwani itasaidia kubadilisha urari wa biashara kati ya nchi hizi mbili ambao kwa sasa inaonesha Oman inauza zaidi nchini Tanzania. Aliwaahidi wafanyabiashara hao kuwa atawakutanisha na Mamlaka husika nchini Tanzania akiwemo Mkurugenzi wa Idara ya Diplomasia ya Uchumi katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Edwin Rutageruka ili kukamilisha taratibu husika. 

Wafanyabiashara hao walielezea malengo yao ya baadaye ni kufanyabiashara ya kusafirisha matunda kutoka nchini kwenda Oman na nchi nyingine za ghuba, jambo ambalo litasaidia wakulima wa Tanzania kupata soko na kuondoa uharibifu wa matunda yanayoharibika kwa kukosa soko.

Balozi wa Tanzania nchini Oman, Mhe. Abdallah Kilima akiwa katika picha ya pamoja na wafanyabishara wa nyama. Kutoka kulia ni Bw. Salem Al Dighaishi - Mkurugenzi wa IKTIMAl Trading Company LLC; Bw. Mohamed S. Aldarai – Mkurugenzi Mwendeshaji wa Abu Suleiman Al-Darai Trading &Services; Dkt. Munawar H. Pardhan – Afisa Mtendaji Mkuu wa Desert Cold Store LLC; na Bw. Aasim M. Pardhan – Mkurugenzi wa Desert Cold Store LLC.

Balozi wa Tanzania nchini Oman, Mhe. Abdallah Kilima akipokea zawadi kutoka kwa Bw. Mohamed S. Aldarai, kiongozi wa ujumbe wa wafanyabiashara ya Nyama nchini Oman. Kushoto ni Bw. Tahir Bakar Khamis – Mkuu wa Utawala, Ubalozi wa Tanzania Oman.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...