Mkuu wa Wilaya ya Lindi Bw Shaibu Ndemanga amewashauri wakulima wa zao la korosho katika mikoa ya Lindi na Mtwara kujiwekea akiba sambamba na kufungua akaunti za akiba kwa ajili ya watoto hatua ambayo ametaja kuwa itawasaidia kujenga nidhamu ya matumizi ya fedha ili kujikwamua na umaskini.

Akizungumza mwishoni mwa wiki mkoani humo wakati wa hafla fupi ya kukabidhi ya zawadi mbambali kwa wakulima wa korosho mkoa wa Mtwara walioibuka washindi wa droo ya tatu ya kampeni ya ‘Vuna Zaidi na NBC Shambani’Bw Ndemanga alisema licha ya wakazi wa mikoa hiyo kupata fedha nyingi kupitia kilimo cha mazao ya korosho na ufuta bado wamekuwa na changamoto za kifedha hususani katika masuala muhimu ikiwemo ada za watoto kutokana na ukata mkubwa unaotokana na wao kutojiwekea akiba.

“Kwa kuwa muda ambao tunapata fedha zitokanazo na kilimo huwa hauendani na muda wa kulipa ada za watoto wetu kumekuwa na ufujaji mkubwa wa fedha kwa matumizi yasiyo na tija sana. Ni kutokana na changamoto hiyo ndio sababu nawaomba sana mjenge utamaduni wa kujiwekea akiba ili isaidie muda sahihi ukifika,’’ alisema

Aliwashauri wakulima hao kufungua akaunti hizo kupitia benki ya NBC kutokana na ukaribu uliopo baina ya wakulima hao na benki hiyo huku akitolea mfano wa akaunti ya NBC Shambani iliyobuniwa mahususi kwa ajili ya wakulima.

“Kwa kuwa jitihada hizi za NBC zimeonesha kuunga mkono juhudi za wakulima na serikali katika kuboresha kilimo cha korosho katika mikoa ya Mtwara na Lindi ni vema pia tuendeleze ushirikiano huu pia hata kwenye akaunti nyingine zikiwemo za akiba na watoto wetu ili kuimarisha zaidi uhusiano wetu na zaidi tukiamini kwamba akufaaye kwa dhiki ndio rafiki wa kweli‘’ aliongeza.

Zaidi, aliwataka wakulima hao kutumia ipasavyo zawadi mbalimbali walizozipata wakulima hao kupitia kampeni hiyo ikiwemo pikipiki, baiskeli, pampu za kupulizia dawa mikorosho ili viweze kuwasaidia katika kujiongezea uzalishaji wa mazao yao sambamba na kujiandaa vema kwa ajili ya msimu ujao.

Kwa upande wake Meneja wa Benki hiyo Kanda ya Kusini Bi Zubeider Haroun alisema kupitia droo hiyo ya pili benki ilitoa zawadi za aina mbalimbali ikiwemo pikipiki, baiskeli, pampu za kupulizia dawa mikorosho, guta (Toyo), pamoja na zawadi za nyingine ikiwemo kanga, mabegi ya shule na madaftari kwa wakulima mmoja mmoja na AMCOS katika mikoa ya Mtwara na Lindi.

“Kampeni hii inalenga kusaidia jitihada zilizowekwa na serikali za kuongeza uzalishaji wa korosho kutoka tani 280,000 zinazozalishwa sasa hadi kufikia tani 700,000 ifikapo mwaka 2025 sambamba na kuwahamasisha wakulima wa korosho kufanya kazi kwa bidii ili kuongeza uzalishaji.’’

“Naendelea kuwahamasisha wakulima waendelee kupitishia fedha zao kupitia benki akaunti ya NBC Shambani ili wawe kwenye nafasi kujishindia zawadi lukuki katika droo zinazofuata,’’ alisema Bi Zubeider

Kwa upande wao washindi wa droo hiyo waliishukuru benki ya NBC kwa kuandaa kwa kampeni hiyo kwa kuwa imekuwa na msaada mkubwa kwao.

“Mbali na zawadi mbalimbali ambazo tumefanikiwa kupata kupitia kampeni hii ya Vuna Zaidi na NBC Shambani’’ tunashukuru pia tumepata hamasa na elimu ya kutosha kuhusu kilimo cha zao hili kibiashara zaidi.’’ Alisema Bw Mustafa Kuwasi mkulima wa korosho mkoa wa Lindi.


Mkuu wa Wilaya ya Lindi  Bw Shaibu Ndemanga  (kulia) na Meneja wa Benki hiyo Kanda ya Kusini Bi Zubeider Haroun (Kushoto) wakiwa kwenye picha ya pamoja na mmoja wa washindi wa droo ya tatu ya kampeni ya Vuna Zaidi na NBC Shambani inayoendeshwa na Benki ya NBC mahususi kwa wakulima wa korosho mikoa ya Lindi na Mtwara, Bw Saidi Likoti aliejishindia pikipiki  (Katikati) wakati wa hafla ya ya kukabidhi ya zawadi mbambali kwa washindi wa kampeni hiyo iliyofanyika mkoani Lindi mwishoni mwa wiki.


Mkuu wa Wilaya ya Lindi  Bw Shaibu Ndemanga  (kushoto) akikabidhi zawadi ya pampu ya kupulizia dawa  mikorosho kwa mmoja wa washindi wa droo ya tatu ya kampeni ya Vuna Zaidi na NBC Shambani inayoendeshwa na Benki ya NBC mahususi kwa wakulima wa korosho mikoa ya Lindi na Mtwara, Bw Mustafa Kuwasi  (Katikati) wakati wa hafla ya ya kukabidhi ya zawadi mbambali kwa washindi wa kampeni hiyo iliyofanyika mkoani Lindi mwishoni mwa wiki. Kulia ni Meneja wa Benki hiyo Kanda ya Kusini Bi Zubeider Haroun.

 

 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...