SERIKALI imetoa wito kwa mabalozi wanaoziwakilisha nchi zao hapa nchini na Wakuu wa Mashirika ya Kimataifa kuunga mkono juhudi za kusaidia upatikanaji wa chanjo ya Uviko 19 kwa Watanzania.

Wito huo umetolewa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula (Mb) alipokutana na mabalozi wanaoziwakilisha nchi zao pamoja na Wakuu wa Mashirika ya Kimataifa Jijini Dar es Salaam.

Waziri Mulamula amewasihi mabalozi hao kuendelea kuungana na Serikali katika jitihada za upatikanaji wa chanjo ya Uviko 19 ambapo amesema kuwa hadi sasa ni watanzania milioni 1.5 wamechanjwa

“Ninawaomba zaidi chanjo nyingine ili watanzania wote waweze kuchanja kwani mwamko wa kuchanja kwa sasa hapa nchini umekuwa mkubwa,” amesema Balozi Mulamula

Pia Waziri Mulamula amewahakikishia kuwa Tanzania inazingatia masula ya demokrasia, utawala bora, utawala wa sheria pamoja na kuheshimu haki za binadamu.

Kwa upande wake kiongozi wa Mabalozi nchini ambaye pia ni Balozi wa Visiwa vya Comoro nchini Mhe. Dkt. Ahmada El Badaoui Mohamed amesema pamoja na mambo mengine, vikao hivyo vimekuwa na manufaa makubwa katika utekelezaji wa majukumu yao hapa nchini.

Nae Waziri wa uchumi wa buluu Zanzibar Mhe. Abdalla Hussein Kombo amesema katika mkutano huo, wamejadili agenda ya uchumi wa buluu ambayo ina vipaumbele vitano ambavyo ni uvuvi na utamaduni, utalii, usafirishaji, usimamizi wa bahari pamoja na nishati.

“Tumewaeleza wenzetu mabalozi vipaumbele vyetu vya uchumi wa buluu na wameonesha nia ya kushirikiana na sisi katika kuendeleza agenda yetu ya Uchumi wa buluu,” amesema Mhe. Kombo

“Pia tumewaeleza kuwa tumemaliza kupitia sera yetu ya uchumi wa buluu na sasa tumeshatekelez mpango wa utekelezaji na sasa tunataka tuone namna gani sisi na wao tunaweza kuanza kuitekeleza agenda yetu ya uchumi wa buluu,” ameongeza Mhe. Kombo

Mkutano huo umehudhuriwa pia na Waziri wa Nishati, Mhe. January Makamba (Mb), Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) na Naibu Waziri wa Madini Mhe. Prof. Shukrani Manya pamoja na Katibu Mkuu na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.
Mawaziri walioshiriki katika kikao kati ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki na Mabalozi na Wakuu wa Mashirika ya Kimataifa wanaoziwakilisha nchi na Taasisi zao hapa nchini kilichofanyika Jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula (Mb) akiongea na mabalozi na Wakuu wa Mashirika ya Kimataifa wanaoziwakilisha nchi na Taasisi zao hapa nchini katika kikao cha pamoja kilichofanyika Jijini Dar es Salaam.
Kiongozi wa Mabalozi nchini ambaye pia ni Balozi wa Visiwa vya Comoro nchini Mhe. Dkt. Ahmada El Badaoui Mohamed akiongea na mabalozi (hawapo pichani) katika kikao cha pamoja kilichoandaliwa na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.
Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Joseph Sokoine akiongea na Mabalozi na Wakuu wa Mashirika ya Kimataifa wanaoziwakilisha nchi na Taasisi zao hapa nchini katika kikao cha pamoja kilichofanyika Jijini Dar es Salaam.
Sehemu ya Uongozi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki ulioshiriki katika kikao cha pamoja kati ya Mabalozi wanaoziwakilisha nchi na Taasisi zao hapa nchini na Uongozi wa Wizara.
Sehemu ya Mabalozi wanaoziwakilisha nchi na Taasisi zao hapa nchini wakifuatilia kikao.
Sehemu ya Mabalozi wanaoziwakilisha nchi na Taasisi zao hapa nchini wakifuatilia kikao.
Sehemu ya Mabalozi wanaoziwakilisha nchi na Taasisi zao hapa nchini wakifuatilia kikao.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...