Watanzania
kutoka sehemu mbalimbali za nchi wakiwamo waliohudhuria tamasha la
muziki wamemshuhudia Abbas Mohamed Mwinyimkuu wa Kawe, jijini Dar es
Salaam, akijishindia zawadi ya bodaboda mpya iliyochezeshwa katika
Uwanja wa Tanganyika Packers, iliyoandaliwa maalum kwa ajili ya wadau na
mashabiki wa muziki kwa kupitia tamasha la Komaa lililoendeshwa chini
ya udhamini mnono wa Kampuni ya Biko, waendeshaji wa bahati nasibu
inayoongoza kutoa washindi wengi nchini Tanzania.
Akizungumza
katika makabidhiano hayo, Mwinyimkuu shabiki na mwanachama maarufu wa
klabu ya Simba, alisema alijaribu kucheza biko kwa mara ya kwanza
uwanjani hapo Jumamosi ya Desemba 4 asubuhi, huku jioni yake akipigiwa
simu ya ushindi.
Mbali na ushindi huo wa droo ya bodaboda kwa
Mwinyimkuu, biko inaendelea kutoa zawadi nono kuanzia sh 2500 hadi Sh
Milioni 5 papo hapo, bila kusahau droo kubwa ya zaidi ya Sh Milioni 40
kila Jumapili ambapo kwa sasa imerahisishwa ambapo Watanzania wanaweza
kucheza live kwa kuingia mtandaoni www.biko.co.tz pamoja na wanaotumia simu za kawaida kwa kuweka namba ya Kampuni ya 505050 na kumbukumbu 2456.
Biko
mchezo unaochezwa kwa njia ya ujumbe mfupi wa maandishi unachezwa kwa
kufanya miamala kuanzia sh 1000 na kuendelea kwa kuchungulia nafasi,
mchezaji anapaswa kuweka namba yake ya simu na fedha kuanzia sh 1000 na
kuendelea na kubonyeza kitufe cha Cheza Sasa kwa ajili ya kuwahi nafasi
za ushindi, huku kila mtu aikiona live jinsi mduara unavyozunguuka na
washindi wanavyopatikana katika bahati nasibu hiyo ya aina yake.
Mshindi
wa bodaboda ya Biko Abbas Mwinyimkuu ambaye pia ni mwanachama wa klabu
ya Simba na Mwenyekiti wa Tawi la Simba Kawe akiwa juu ya pikipiki
aliyoshinda kutoka kwenye bahati nasibu ya Biko Jumamosi iliyopita
katika Viwanja vya Tanganyika Packers, Kawe, jijini Dar es Salaam,
katika Tamasha la Komaa Concert lililoandaliwa na EFM Radio, huku Biko
wakiwa sehemu ya wadhamini wa tamasha hilo. Picha na Mpigapicha wetu.
Mshindi
wa bodaboda ya Biko Abbas Mwinyimkuu ambaye pia ni mwanachama wa klabu
ya Simba na Mwenyekiti wa Tawi la Simba Kawe, akipokea karatasi muhimu
za umiliki wa hicho cha usafiri kutoka kwa waendeshaji wa bahati nasibu
ya Biko ikiwa ni zawadi maalum iliyoandaliwa katika Tamasha la muziki la
Komaa Concert lililofanyika viwanja vya Tanganyika Packers, Kawe,
jijini Dar es Salaam, chini ya EFM Radio kwa udhamini mnono wa Biko.
Anayekabidhi nyaraka hizo ni Meneja Masoko wa Biko Goodhope Heaven na
kushuhudiwa na mtangazaji wa EFM, Jackilne Charles kushoto. Picha na
Mpigapicha Wetu.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...