Balozi wa Tanzania nchini Marekani na Mexico Balozi Elsie Kanza amekutana kwa mazungumzo na Meya wa mji wa Dallas, Meya Eric Johsnon pamoja na kufanya mazungumzo na jumuiya ya Watanzania (Diaspora) waishio Marekani na Mexico.




BALOZI wa Tanzania nchini Marekani na Mexico Balozi Elsie Kanza amekutana kwa mazungumzo na Meya wa mji wa Dallas, Meya Eric Johsnon pamoja na kufanya mazungumzo na jumuiya ya Watanzania (Diaspora) waishio Marekani na Mexico.

Mazungumzo kati ya Balozi Kanza na Meya Eric Johnson yalilenga katika kuimarisha uchumi wa kidiplomasia hususan katika sekta za utalii,biashara na uwekezaji ambapo amemuomba Meya Eric kuwahasisha wafanyabiashara na wawekezaji kuja Tanzania kuwekeza kutokana na uwepo wa fursa nyingi huku mazingira ya biashara na uwekezaji yakiwa yameboreshwa kwa kuondoa kodi kero tangu serikali ya awamu ya Sita chini ya uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan uingie madarakani.

Katika mkutano na Watanzania waishio Marekani na Mexico na kuzungumzia juu ya namna ya kutangaza fursa mbalimbali za biashara na uwekezaji zilizopo Tanzania pamoja na kuweka mikakati ya kuwavutia watalii wengi kwenda Tanzania kutembelea vivutia mbalimbali vya uwekezaji.

Pia Balozi Kanza amefanya mazungumzo na Watanzania (diaspora) waishio Marekani katika Majiji ya Texas na Houston,kwa lengo la kujitambulisha katika jumuiya hiyo na kujadiliana masuala mtambuka kuhusu maendeleo ya Tanzania.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...