Na Bakari Madjeshi, Michuzi TV

BIBI mmoja anayesadikiwa kuwa na umri wa miaka 86 aliyefahamika kwa jina la Asia Ally Mwangaza amefariki dunia baada ya kuanguka kwa Ghorofa na kufunikwa na kifusi, eneo la Goba kwa Awadhi jijini Dar es Salaam Desemba 6, 2021, tukio lililotokea Majira ya saa 10 jioni.

Kifo cha Bibi huyo kimethibitishwa na Mtoto wake, Ally Issa wakati akizungumza na Michuzi Blog na Michuzi TV kwenye eneo hilo la tukio ambapo uokoaji unaendelea.

Issa amesema akiwa nje ya nyumba hiyo alishuhudia tukio hilo la kuanguka kwa Ghorofa hilo lililopo karibu ya nyumba aliyokuwa anaishi Mama yake, marehemu Bi. Asia.

“Aliniagiza Unga wa Ugali, lakini hakuweza kusonga hadi umauti ulimkuta akiwa ndani ya nyumba ambayo alikuwa anaishi, alienda kuchukua Chaji ya Simu ndani, hajatoka kuchukua Chaji, Jengo likadondoka, amesema Issa.

Ally Issa ameeleza kuwa Kiwanja hicho palipokuwa na Ujenzi wa Ghorofa hilo liloanguka, ilikuwa sehemu yake na aliwahi kupauza kwa mtu mwengine ambaye naye aliuza eneo hilo kwa tajiri huyo wa Ghorofa hilo mwaka huu wa 2021.

Serikali kupitia Kikosi cha Zimamoto na Uokoaji Mkoa wa Kinondoni wameendelea na zoezi la uokoaji ikiwa ni kutafuta na kuangalia miili ya maiti hao ambapo hadi sasa, inasadikiwa kuna baadhi ya watu wamefukiwa na Kifusi hicho, wakiwemo Mafundi Wasaidizi ujenzi sambamba na Mwanamke mmoja anayesadikiwa kuwa Mama Ntilie ambaye ametwajwa alikuwa akiwaletea chakula mara kwa mara Mafundi hao.

Kaimu Kamanda wa Kikosi hicho, Mkaguzi Isaac Njombe ameeleza kuwa wanaendelea na kutafuta miili mingine kadri watakapoona kuna haja ya kuendelea na zoezi hilo la uokoaji, huku akiwashukuru Wananchi wa maeneo hayo kutoa ushirikiano wengine wakisaidia kuokoa na kutafuta miili mingine inayotajwa kubaki baada ya kuangukiwa na Kifusi.

Mkaguzi Njombe amesema wameokoa maisha ya Watu 17 wakiwa majeruhi huku walitoka miili ya Watu wanne ambao wamepoteza maisha kutokana na ajali hiyo ya kuporomoka kwa Ghorofa hilo.




Askari wa Kikosi cha Zimamoto na Uokoaji wakiendelea na zoezi la Uokoaji katika eneo la Goba Kwa Awadhi ambapo limeanguka Ghorofa na kusababisha vifo vya Watu wapatao wanne huku miili mengine ikiendelea kutafutwa kutokana na kufukiwa na Kifusi katika eneo hilo.



Baadhi ya Wananchi wa eneo la Goba Kwa Awadhi, Askari wa Kikosi cha Zimamoto na Uokoaji sambamba na Watu wa ‘Red Cross’ wakiwa na kazi kubwa ya kushirikiana kuokoa miili ya watu waliofariki dunia kutokana na kufukiwa na Kifusi baada ya kuporomoka kwa Ghorofa. (Picha zote na Bakari Madjeshi).


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...