Mkuu wa wilaya ya Arusha Mjini Mh,Said Mtanda amefanya ziara katika masoko yaliyopo katika wilaya yake.

Ziara hiyo ikiwa na lengo la kujionea miundombinu katika masoko hayo ambapo ametoa maelekezo ya kuhakikisha kuwa vyoo vyote vinakamilika na kutumika ipasavyo ili afya za wafanyabiashara hao ziwe salama.

Pia mh.Mtanda alisema kuwa miundo mbinu katika masoko hayo ni lazima iboreshwe haswa katika kipindi hiki cha mvua ili pasiwepo na kikwazo cha wafanyabiashara kufanya shughuli zao.

“Nitatuma mhandisi aje kuangalia maeneo ambayo yanavuja na kisha alete bajeti ya kiasi kinachohitajika ili tuweze kuweka mapaa na kuhakikisha mnafanya shughuli zenu katika mazingira mazuri”Alisema Mtanda

Aidha alitumia fursa hiyo kusikiliza kero za wafanyabiashara na kutatua changamotombali mbali zinazowakabili.

Masoko ambayo mheshimiwa Mtanda alitembelea ni pamoja na Kilombero,Mbauda na Soko namba 68 ambapo pia alikagua miundo mbinu iliyopo sokoni hapo.






Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...