Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
MKUU
wa wilaya ya Ilala, Mheshimiwa Ng'wilabuzu Ndwata Ludigija, amechagiza
utolewaji wa zawadi za mbuzi za sikukuu ya Christmass na Mwaka mpya
zinazotolewa kwa wingi katika ushindi wa papo kwa hapo wa Bahati nasibu
ya Biko, akisema zitapunguza makali ya maisha kwa Watanzania
watakaofanikiwa kushinda kwenye droo hizo.
Mheshimiwa Ludigija
aliyasema hayo wakati wa makabidhiano ya hundi ya sh Milioni 10 kwa
Mikidadi Kaimu Ngoo wa Chanika, wilayani Ilala, mkoani Dar es Salaam,
aliyeshinda kwenye droo ya Jumapili na kuwa miongoni mwa Watanzania
wengi wanaobukua mamilioni ya Biko, ambapo katika droo za papo kwa hapo,
sh laki mbili mbili zitamwagika kama sehemu ya ununuaji wa mbuzi za
sikukuu za mwisho wa mwaka.
Mchezo wa biko unachezwa live mtandaoni kwa kuingia www.biko.co.tz
bila kusahau wale wanaotumia njia ya kawaida kwa kucheza kwa namba ya
Kampuni 505050 na kumbukumbu 2456 au neno biko, huku kianzio cha kucheza
kikiwa sh 1000 na kuendelea.
Biko ni mchezo wa kubahatisha
unaoongoza kutoa fedha nyingi kwa Watanzania, ambapo zwadi za papo kwa
hapo zinatoka kila sekunde moja kuanzia sh 2500 hadi milioni 5 papo hapo
bila kusahau kutoa zawadi ya hadi sh milioni 40 kila Jumapili ambapo
mbali na kucheza kwa namba ya Kampuni 505050 na kumbukumbu 2456, pia
watu wanaweza kucheza live kwa kuingia www.biko.co.tz.
Mkuu wa wilaya Ilala, Mheshimiwa Ng'wilabuzu Ndwata Ludigija akifurahia na mshindi wa milioni 10 wa Biko, Mikidadi Kaimu Ngoo alipomtembelea ofisini kwake kumkabidhi hundi yake ya ushindi wa Biko. Picha na Mpigapicha Wetu.


Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...