Na. John Mapepele
Naibu
Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo amekitaka chama cha kuogelea
nchini kushirikisha mikoa yote nchini ili kupata waogeleaji wenye
vipaji watakaoiwakilisha vema Tanzania kwenye mashindano ya kimataifa.
Mhe.
Gekul ameyasema haya leo Disemba 4, 2021jijini Dar es Salaam
allipoambatana na Kaimu Katibu Mtendaji wa Baraza la Michezo la Taifa(
BMT) Neema Msitha kuikabidhi bendera na kuiaga timu ya Tanzania
inayokwenda kushiriki mashindano ya Afrika ya kuogelea nchini Uganda.
Aidha, amewapongeza wazazi kwa kuwaruhusu watoto kushiriki katika mchezo huu.
"Niwapongeze
wazazi kwa mwamko mkubwa wa kuwarushusu watoto kujiunga kwenye mchezo
huu, hii itasaidia kupata vipawa na vipaji vingi " amefafanua Mhe. Gekul
Amesema Serikali imeshaandaa Mpango Mkakati wa miaka kumi wa kuinua na kuendeleza michezo ili kuinua michezo.
Naye
Msitha amemweleza Mhe. Naibu Waziri kuwa chama cha mchezo wa kuogelea
ni miongoni mwa vyama vya michezo inayofanya kazi nzuri ya kuinua
mchezo huu hapa nchini.
Kiongozi wa timu hiyo Inviolata Itatilo amesema nchi zaidi ya kumi za Afrika zinashiriki mashindano haya nchini Uganda.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...