Na Muhidin Amri,Songea

MKUU wa mkoa wa Ruvuma Brigedia Jenerali Wilbert Ibuge,ameipongeza Halmashauri ya wilaya ya Songea kwa  kazi nzuri  katika kutekeleza miradi ya ujenzi wa vyumba vya madarasa yanayojengwa katika shule mbalimbali za sekondari.

Jenerali Ibuge ametoa pongezi hizo kwa nyakati tofauti, wakati akikagua ujenzi wa vyumba vya madarasa vinavyojengwa chini ya mpango wa maendeleo na ustawi wa Taifa na mapambano dhidi ya Covid-19 katika shule ya Sekondari Maposeni na Mpitimbi.

“Mkurugenzi  na wataalam  wako nawapongeza sana kwa kazi nzuri mnayoifanya,nimepita maeneo mbalimbali kwa ajili ya kuangalia kazi ya ujenzi wa miradi hii ya Covid-19 lakini nyinyi mmenifurahisha sana”alisema Ibuge.

Alisema, licha ya majengo yake kufikia hatua nzuri ya utekelezaji wake,pia yamejengwa kwa ubora wa hali ya juu na kuzitaka Halmashauri nyingine za mkoa huo kwenda kujifunza  namna ya utekelezaji wa miradi hiyo katika Halmashauri ya wilaya ya Songea.

Alisema,ataendelea kusimamia  fedha zinazoletwa  kwa ajili ya kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo katika mkoa huo na hatokubali hata kidogo kuona baadhi ya miradi inajengwa chini ya kiwango.

Hata hivyo,amemuagiza Mhandisi wa ujenzi kufanya marekebisho madogo  kwenye ngazi za kuingia darasani na ofisi za walimu ili  watu wenye mahitaji maalum(walemavu) ili iwe rahisi  nao.

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya Songea Neema Maghembe alisema, kwa mwaka wa fedha 2021/2022  Halmashauri hiyo imepokea jumla ya Sh. 500,000,000.00 kwa ajili ya ujenzi wa wa vituo  vya afya viwili  vya Liganga na Kilagano ambapo kila kituo kimepatiwa Sh. 250,000,000.00.

Aidha alisema,Halmashauri imepokea  Sh. 90,000,000.00 kujenga nyumba tatu za watumishi katika kituo cha afya Matimila ambapo ujenzi wake upo katika hatua mbalimbali za utekelezaji.

Akizungumzia ujenzi wa vyumba vya madarasa alisema, wamepokea Sh.380,000,000.00 kwa ajili ya ujenzi wa vyumba vya madarasa  katika vituo shikizi vya shule za msingi tano ambazo ni Jenister,Mhimbasi,Lihulu,Lunyele  na Ligunga.

Pia alimueleza Mkuu wa mkoa kuwa,Halmashauri imepokea mgao wa Sh. 920,000,000.00 ambazo zimeanza kutumika kujenga vyumba 46 vya madarasa kwenye shule 16 za Sekondari.

Maghembe alisema,utekelezaji wa mkiradi hiyo ipo katika hatua mbalimbali ambapo ujenzi wa vyumba viwili katika ya Mpitimbi upo katika hatua ya umaliziaji, na shule saba zenye jumla ya vyumba 17 tayari zimeezekwa bati pamoja na upigaji wa lipu ndani na  nje.

Kwa mujibu wa Maghembe,kazi za ujenzi wa vyumba vya madarasa katika shule shikizi na shule za sekondari unaendelea vizuri na umefikia asilimia 70.


Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Songea vijijini mkoani Ruvuma  Neema Maghembe kulia,akitoa taarifa ya ujenzi wa vyumba vya madarasa kwa mkuu wa mkoa huo Brigedia Jenerali Wilbert Ibuge jana ambapo ujenzi wa vyumba vya madarasa vinavyojengwa chini ya mpango wa maendeleo na ustawi wa Taifa na mapambano dhidi ya Covid 19 umefikia asilimia 7.Picha na Muhidin Amri.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...