KAIMU Mkurugenzi wa Idara ya Miliki Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) Said Mndeme ameridhishwa na kasi  ya ujenzi  wa mradi wa nyumba 3500 na nyumba 20 za viongozi zinazojengwa Jijini Dodoma  na Wakala huo.

Akizungumza na Waandishi wa Habari leo Desemba 3,2021 Jijini Dodoma mara baada ya kukagua ujenzi wa nyumba hizo,Kaimu Mkurugenzi huyo ameridhishwa na jinsi Wakala huo ulivyojipanga kutekeleza miradi hiyo kwa kuwa na vifaa vya kutosha na vya uhakika.

“Tumeridhika kwa jinsi ambavyo  wamejipanga tuna Cementi ya kutosha nondo za kutosha haya ni maono ya wakala,hatuna sababu ya kuwa na vikwazo vyovyote binafsi nimeridhika na nimefurahi  katika kuhakikisha tunapunguza gharama na ubora unakuwa mzuri   mashine ya kisasa ya kuchakata zege.

“Tumeona Kiwanda kingine cha uzalishaji wa tofali hii itatisaidia tofali zenye ubora tumeambiwa kiwanda kinauwezo wa  kuzalisha tofali 6000,”amesema.

Amesema mradi wa Nzuguni unaenda kwa kasi ambapo zitajengwa nyumba 3500 ambapo amedai awamu ya kwanza zinajengwa  nyumba 150 na kwamba nyumba  86 zimeanza kujengwa.

“Nyumba hizi 3500 zitakuwa ni za kisasa kutakuwa na ujenzi maghorofa  100  na nyumba kubwa 200 na nyumba za saizi ya kati 1400, maghorofa yatakuwa nyumba  tofauti tofauti 800 na za size za chini nyumba 1000.

Aidha,amesema katika eneo hilo kutakuwa na huduma za kijamii ambapo kutajengwa shule za awali tano,nyumba za ibada misikiti na makanisa,Soko na kituo cha biashara.  

Kuhusiana na nyumba 20 za viongozi katika eneo la Kisasa Jijini Dodoma,Kaimu Mkurugenzi huyo wa Miliki amesema zimeboreshwa na  kuongezewa ubunifu ikiwa ni pamoja na vyumba vyote kuwa Master bedroom

“Lakini tumeona jitihada kubwa ambazo zimefanyika nyumba hizi zinajengwa katika nyumba 300 katika eneo la  Kisasa lakini nyumba hizi sasa hivi zimeboreshwa kwa kiasi kikubwa Kwanza nyumba hizi muonekano ni tofauti na zile nyumba  300 ambazo zilijengwa za sasa hivi kila chumba kina choo,”amesema.

Kwa upande wake,Kaimu Meneja Maendeleo ya Miliki TBA,Suzan Ulula amesema wanaamini watafikia malengo ambayo wamejiwekea ikiwa ni pamoja na kukamilisha kwa wakati ujenzi wa nyumba hizo.

“Baada ya kutembelea Nzuguni na Kisasa tunaamini tutafikia malengo wakala ambayo imeyaweka kwa watumishi wa Serikali.Kwa mkoa wa Dodoma tunamaeneo  mengine Iyumbu na katika Mikoa mbalimbali Arusha na Dar tunategemea tutaendelea na sehemu zingine,”amesema.

Naye,Msimamizi wa Mradi wa ujenzi wa nyumba 3500 Nzuguni Jijini Dodoma,Fedrick Jackson amesema ujenzi huo ulianza  Oktoba 25,2021 ambapo amedai matarajio ni kwa nyumba zote 150 ziwe zimekamilika  Septemba 30 mwakani.

“Kwa matarajio ya miezi mitatu mitatu kwa nyumba 50 lakini tunajaribu kukimbizana ili tuzikamilishe nyingi kwa wakati mmoja hizi nyumba 86 ambazo tumeanza nazo mwezi wa tatu mwishoni kuelekea wanne  mwanzoni tunatakiwa tuwe tumeishazimaliza.

“Lakini wakati huo zile nyumba 64 ambazo zitatutimizia nyumba 150 zinatakiwa ziwe mpaka mwezi wa sita ziwe zimekamilika.Hapa kila kitu kimepimwa maabara na namna ujenzi unavyokuwa tunasimamia na kupitia  mara kwa mara kwa maana kile cha maabara tunakipeleka kupimwa,”amesema.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...