Na Amiri Kilagalila,Njombe
KAMATI ya siasa ya Chama cha Mapinduzi (CCM) wilaya ya Njombe imekagua madarasa 13 kati ya madarasa 28 yanayogalimu shilingi milioni 560 yanayojengwa kwa msaada wa fedha za maendeleo UVIKO,mwenyekiti wa Chama hicho wilaya Mzee Edward Mgaya kwa niaba ya kamati amesema wameridhishwa na maendeleo ya ujenzi wa miradi hiyo.
Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Njombe Bi,Sharifa Nabalang’anya akishiriki katika kazi pamoja na wananchi wa Mtwango wanaoendelea na ujezni wa madarasa ya shule ya sekondari Sovi.
G:Kamati ya siasa ya ikipokea taarifa ya ujenzi wa maadara matatu katika shule ya sekondari Kidegembye yaliyotengewa shilingi milioni 60 ujezni upo kwenye hatua ya upigaji wa Plasta.
Kamati ya siasa ikikagua maendeleo ya ujenzi wa madarasa mawili yanayojengwa kwa fedha za Uviko katika shule ya sekondari J.M Makweta iliyopo kata ya Kichiwa yaliyotengewa milioni 40.Madarasa yapo katika hatua ya upigaji wa Plasta.
Wajumbe wa kamati ya siasa wakikagua maendeleo ya ujenzi wa madarasa manne katika shule ya sekondari ya wasichana ya Manyunyu iliyoko Matembwe shule hiyo imetengewa shilingi milioni 80.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...