Kiwanda kipya
na cha kwanza cha kutengeneza na kuunganisha magari nchini Tanzania GF
cha Vehicles Assemblers (GFA) kilichopo Kibaha katika mkoa wa Pwani leo
kimeendesha zoezi la kuchangia damu kwa hiari katika hospitali ya Tumbi
mkoani humo.
Tukiwa
tunaelekea katika msimu wa sikukuu za mwishoi wa Mwaka kumekuwa na
ajali nyingi nchini zimekuwa zikitokea hali iliyopelekea kuzalisha
majerui wengi wanaohitaji kuwekewa damu na hivyo benki zetu za damu
katika hospitali kuhelemewa.
Kwa kutambua Kiwanda cha kutengeneza
na kuunganisha magari nchini Tanzania GF cha Vehicles Assemblers (GFA)
kimeamua kuendesha zoezzin la kuchangia damu kwa hiari lililofanywa na
wafanyakazi wake katika kiwanda hicho
Akizungumza wakati wa wa
zoezi hilo Meneja Mkuu wa Kiwanda cha hicho, Ezra Mereng alisema wao
kama kampuni wamekua na kawaida ya kurejesha kwa jamii kile kidogo
wanachokipata na katika hili tumekua tukichangia madawati katika shule
na tuliwahiu kupeleka misaada mbali mbali katika vituo vya yatima na
hivi leo tumeamua kujitolea Damu mimi na wafanyakazi wenzangu
Kwa
upande wa Tumbi akizungumza wakati wa zoeziu hili Afisa ustawi wa
Kitengo cha Damu Hospitali hiyo Feliciana Mmasi alisema wao kama tumbi
wanamahitaji makubwa ya damu ukizingatia hospitali hiyo inahudumia
wagonjwa mbali mbali watokanao na ajali.
Zinazotokea katika
mkoa huo kufuatia kuwa kiunganishi cha mikoa mingi ,pia mahitaji kwa
mama wajawazito hali inayopelekea matumizi kwa siku ya damu ni kati ya
Unit 10-15 hivyo kwa zoezi hili la kuchangia lililofanywa na kiwanda
hiki cha magari tumekusanya Unit 15.
Tunashukuru
kutokana na uhamasishaji kuwa mdogo na elimu ya uchangiaji damu
kutowafikia wananchi wito wangu kwa wananch ni kwamba wajenge tabia ya
kuchania damu ili kuokoa wenzetu wenye mahitaji.
Nae Baraka
Samsoni mmoja wa wachangiaji damu alisema anajisikia faraja kwa
kuchangia damu hii ni mara ya kwanza lakini alikuwa anahofia kama akitoa
damu basi anaweza akapata madhara lakini ni tofauti kabisa na
nilivyokuwa nadhani.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...