Na.WAMJW,DSM
Maabara za Tanzania zina uwezo wa kupima UVIKO-19 na majibu yake yana ubora unaokubalika kikanda na kidunia kwa mujibu wa taarifa ya EAC na Vigezo vya Shirika la Afya Duniani (WHO)
Hayo yamebainishwa na Mganga Mkuu wa Serikali Dkt. Aifello Sichalwe wakati wa ziara maalum ya kukagua mwenendo wa huduma za upimaji wa UVIKO-19 ndani ya uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere(JNIA)
Dkt. Sichalwe amesema kuwa Tanzania ni moja kati ya nchi 6 za Afrika Mashariki ambayo maabara zake zimefanyiwa utambuzi na kukubalika na jumuiya hiyo. Katika Taarifa ya ya tathmini ya Ubora wa Huduma za upimaji wa UVIKO-19 iliyowasilishwa mwezi Novemba na Jumuiya ya Afrika Mashariki, Maabara ya Taifa imepata asilimia 100 ya vipimo vya Ubora huku Maabara nyingine za Kanda zikiwa zimepata asilimia 96-98 kiwango ambacho ni Cha juu ukilinganisha na kiwango Cha asilimia 80 kilichowekwa na Shirika la Afya Duniani (WHO)
Hata hivyo amesema kuwa Wizara kupitia Maabara kuu ya Taifa ya Jamii imefunga mashine nyingine kubwa na za kisasa kwa ajili ya kupima kipimo cha haraka cha UVIKO-19(PCR ) kwa wasafiri wanaoenda nchi za Falme za Kiarabu ikiwemo Dubai.
Amesema kufuatia tangazo la Falme za Kiarabu kutaka wasafiri wanaotokea Tanzania kwenda Dubai, kupata vipimo vya masaa 48 na kisha kumalizia na kipimo cha masaa sita (6) kabla ya safari.
"Nimefika hapa uwanja wa ndege kujionea hali halisi na hali ni nzuri, mashine za kutosha zipo na timu inaendelea na kazi na pia nimeshuhudia eneo la tenti nje ya uwanja ambapo wateja watakapokuwa wanaanzia kupatiwa huduma. Kikubwa wafike mapema na kwa wakati kulingana na muda wa safari zao." alisema Mganga Mkuu Dkt. Sichalwe.
Kwa upande wake, Meneja wa huduma za afya mipakani, ambaye pia ni msimamizi mkuu wa huduma za afya katika uwanja wa ndege wa Julius Nyerere Dar es Salaam, Bw. Remidius Kakuru alieleza kuwa, Wizara imeendelea kupima wasafri wanaoingia na wanaotoka nchini na zoezi linaenda vizuri.
"Niwasisitize wasafiri kuwa, huduma imeanza kutolewa tokea tarehe 16 mwezi huu na tayari tunaendelea na upimaji kwa wasafiri wanaokwenda Dubai.
Tunawasisitizia wasafiri wajitahidi wafike mapema uwanja wa ndege ikiwezekana masaa saba kabla ya safari zao na gharama hizi za kipimo cha pili ni sawa na ile ya kipimo cha kwanza." Alisema Kakuru.
Nae Mwandisi Barton Komba ambaye ni Meneja wa JNI Terminal 3, alishukuru Serikali kwa kuwezesha mashine hizo kwa haraka na abiria wote kuweza kupima ndani ya uwanja huo.
"Kwa niaba ya mamlaka ya uwanja wa ndege, tunapongeza juhudi za Serikali kwa kuwezesha kuletwa mashine ndani ya siku tatu na abiria wanapatiwa huduma na sasa ndege ya Emirates itaanza kuondoka kwend huko Dubai na tutarudi kwenye shughuli yetu kama ilivyo awali." Alisema Komba.
Katika kuhakikisha ndege hizo za Falme za Kiarabu zinaendelea na safari zake hapa nchini, Meneja wa ndege za Emirates Tanzania uwanja wa ndege wa Terminal 3, Bw. Aboubakar Juma amemhakikishia Mganga mkuu wa Serikali kuwa, Emirates itaendelea na safari zake ambapo kwa sasa wanasubiria kukamilika kwa taratibu ndani ya uwanja huo.
"Tunapenda kuujulisha umma kwamba, kutokana na matakwa mapya ambavyo vilevile yamekuja ghafla kutoka Falme za Kiarabu kwa wasafiri kutoka Tanzania wanaokwenda Dubai, wataitajika kupima mara mbili, ikiwemo PCR covid test masaa sita kabla ya safari.
"Tunapongeza uongozi wa Wizara ya Afya kwa kuchukua hatua thabiti sana na za haraka kuhakikisha ili zoezi linaenda vizuri. Hapa nje tumeona tenti kubwa limefungwa na sehemu ya kuchukuliwa vipimo, ambapo tutakapokuwa tayari kutangaza kwamba kusafiri wateja wote wanaokwnda Dubai watahitajika kufika uwanja wa ndege masaa saba kabla ya safari wakiwa na 'covid test' zao za kawaida zisio chini ya masaa 48 na wakifika hapa watapitia eneo hili wakiwa wameshalipa 'USD 50' kupitia malipo ya mtandaoni ilikupunguza usumbufu hapa
Aidha, amesema baada ya taratibu, watatumiwa majibu yao kupitia simu zao kwa kupitia mtandao wa WhatsApp ama email kisha taratibu zingine na safari.
Wasafiri wanatakiwa kufanya miahadi ya safari zao 'booking' kupitia mtandaoni katika;
https://pimacovid.moh.go.tz/#/booking na kufanya malipo na kisha kuchagua kituo cha kupima na kupata cheti ambacho kinakuwa tayari ndani ya masaa 48.
Nae Kaimu Mkurugenzi wa mahabara kuu ya taifa, amewaomba wasafiri ambao wanatakiwa kupima uwanja wa ndege ni wale tu wanaokwenda ama kupitia Dubai pekee na wale wengine watatumia utaratibu wao wa kawaida.
"Tulipata mahitaji hayo ya Emites na tukafunga vifaa hapa uwanjani na hadi sasa tayari tumepima abiria Sabina na moja.Abiria wakifika mapema zaidi itasaidia wao kuwahi safari zao na pia wanatakiwa walipie mtandaoni ilikuepuka usumbufu.
Wataalam wa Maabara Kuu ya Taifa ya Jamii wakiwa katika majukumu yao katika eneo maalum la kupimia sampuli za UVIKO 19 (PCR) ndani ya uwanja wa ndege wa JNIA terminal 3.Mganga Mkuu wa Serikali Dkt. Aifelo Sichalwe akiwa katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA terminal 3 na kukagua miundombinu ya kukabiliana na UVIKO-19 kwa abiria wanaoingia na kutoka.
Wataalam wa Maabara Kuu ya Taifa ya Jamii wakiwa katika majukumu yao katika eneo maalum la kupimia sampuli za UVIKO 19 (PCR) ndani ya uwanja wa ndege wa JNIA terminal 3.
Sehemu za mashine za kisasa ilizofungwa na Maabara Kuu ya Taifa ya Jamii katika eneo maalum la kupimia sampuli za UVIKO 19 (PCR) ndani ya uwanja wa ndege wa JNIA terminal 3
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...