Na Mwandishi Wetu,Morogoro

MAOFISA na askari 14 wa Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA), wamevishwa vyeo vipya baada ya kupandishwa na wengine kubadilishiwa madaraja ya utumishi.

Katika hafla hiyo iliyofanyika leo Desemba 18, 2021, katika Makao Makuu ya TAWA, Morogoro,Mgeni rasmi Naibu Kamishna wa Huduma (TAWA), Prosper Kyssima, akimwakilisha Kaimu Kamishna wa Uhifadhi Mabula Misungwi Nyanda, amewataka maofisa na askari hao kuvitendea haki vyeo hivyo kwa kutimiza majukumu yao kwa weledi katika maeneo yao ya kazi huku wakizingatia nidhamu ya kijeshi kwa mapana yake.

Pia amewaelekeza maafisa na askari wa TAWA kuzingatia nidhamu katika jeshi ikiwa ni pamoja na kuzingatia mahudhurio ya paredi zote zilizowekwa kwa mujibu wa utaratibu.

Amesisitiza, wanatakiwa kumheshimu aliyewazidi na waliyemzidi cheo, kuwa nadhifu wa mavazi na mwenendo wa jumla mahali pa kazi na katika jamii.

"Ni imani yangu kwamba vyeo mlivyovishwa kijeshi vitawaongezea nidhamu, ujasiri na kujiamini pale mtakapokuwa mnatekeleza majukumu yenu," amesema Kyssima.

Kwa upande wake Kamishna Msaidizi Mwandamizi Operesheni Mlage Kabange, amesema TAWA itaendelea na utekelezaji wa agizo la serikali la kubadili mfumo wa uendeshaji kutoka mtindo wa kiraia kwenda mfumo wa kijeshi, kwa maafisa na askari wake maeneo yote.

Amesema katika kuthibitisha azma hiyo, hadi sasa kuna maafisa na askari 150 wanaoendelea na mafunzo katika Chuo cha Likuyu Sekamaganga, ambao wanatarajiwa kuhitimu Desemba 22, mwaka huu.



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...