Na Jane Edward, Arusha

MKUU wa Mkoa wa Arusha John Mongela amekiomba Chuo Cha uhasibu mkoani Arusha kuendelea kujipambanua zaidi katika kufanya makongamano yenye mashiko na yanayohusiana na mustakabili wa taifa yatakayo onyesha picha ya kikanda.

Mongela ameyasema hayo wakati wa ufunguzi wa kongamano la maadhimisho ya miaka 60 ya Uhuru wa Tanzania Bara lililoandaliwa na Chuo Cha uhasibu Arusha.

"Nakipongeza Chuo kwa kuandaa kongamano lenye mada ya utalii na kwamba anakiomba chuo hicho kiendelee kujipambanua kufanya makongamano ya kidunia na kikanda," amesema Mongela.

Aidha Mongela amewataka vijana kujitambua ,kujithamini na kujiongeza kwa kuwa uongozi Ni njia ya kuwafanya wafikie hatua ya maendeleo.

Kwa upande wake Mkuu wa Chuo cha Uhasibu Arusha profesa Eliamani Sedoyeka amesema wamefanya kongamano Hilo kufuatia maelekezo waliyopewa na serikali ya kuwataka kufanya kongamano ngazi ya mkoa la maadhimisho ya miaka 60 linaloendana na dhima ya uchumi .

Profesa Sedoyeka amesema lengo Ni kukaa na wadau na kujadiliana na kuangalia changamoto na faida zilizopo katika sekta ya utalii kwa kipindi Cha miaka 60.

"Sisi kama chuo cha uhasibu Arusha tupo ndani ya kitovu cha utalii ambapo ni hapa Arusha na fursa za utalii zipo na kongamano hili ni kuwaonyesha vijana wa chuo chetu kuona fursa na kufahamu maliasili zilizopo,"amesema Profesa

Wakati huo huo Mwenyekiti wa Chama cha Mawakala wa Utalii Tanzania (Tato ) Wilbard Chambulo amewataka vijana kuwekeza zaidi katika sekta ya utalii kwa kuwa ni sekta yenye biashara kubwa.

"Mimi kama mfanyabiashara ya Utalii Mkubwa hapa nchini ndoto yangu ni kuona vijana kama nyie mnaingia kwenye sekta hii na sio kuachia watu kutoka mataifa mengine kunufaika na rasilimali zetu,"amesema Chambulo

Amekihakikishia Chuo hicho kuwa wao kama wakala wa Utalii wako tayari kutoa ushirikiano kwa Chuo hicho katika kufahamu masuala ya Utalii na fursa zake.
Mkuu wa Chuo cha Uhasibu Arusha Profesa Eliaman Sedoyeka, akitoa neno la utangulizi kabla ya ufunguzi wa kongamano la utalii miaka 60 ya Uhuru.
Mkuu wa Mkoa wa Arusha John Mongela, akifungua kongamano la maadhimisho ya miaka 60 ya uhuru katika kujadili mafanikio na changamoto katika sekta ya Utalii.

Willbad Chambulo Mwenyekiti wa chama cha wakala wa utalii Tanzania(TATO)akiwaasa vijana kuingia kwenye biashara ya Utalii .

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...