Na John Walter-Manyara
WAZIRI wa Afya, Maendeleo ya jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk.Dorothy akizungumza jijini Dodoma kwenye kilele cha maadhimisho ya wiki ya usafi wa mazingira Tanzania na Mkutano Mkuu wa mwaka wa wadau wa Afya ya Mazingira ametangaza mikoa iliyoongoza katika mashindano hayo.
Akitangaza matokeo hayo ya mashindano ya taifa ya usafi wa mazingira kwa mwaka 2021, ameutangaza Mkoa wa Manyara, Katavi na Dodoma kuwa vinara wa usafi.
Kwa upande wa Halmashauri za Majiji ni Tanga, Arusha na Mwanza, huku Manispaa ya Moshi, Iringa na Kinondoni pia zikifanya vizuri.
Miji ni Njombe, Tunduma na Babati na kwa upande wa Halmashauri za Wilaya ni Njombe, Makete na Moshi.
Naye Mkurugenzi wa Idara ya Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe Ofisi ya Rais TAMISEMI, Dkt. Ntuli Kapologwe amesema wataalamu wa afya mazingira wataongezwa ili watekeleze majukumu yao kwa weledi na kwamba upandishaji madaraja kwa watumishi ambao bado utafanyika kwa kuwa maelekezo yalishatolewa.


Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...