NA VICTOR MAKINDA:
MVOMERO
MKUU wa Wilaya ya
Mvomero Mkoani Morogoro, Halima Okash,
ameziomba Asasi za Kiraia (AZAKI) zinazofanya shughuli zake wilayani hapa, kusaidiana
na viongozi wa ngazi viongozi wa ngazi
mbali mbali pamoja na kamati ya ulinzi
na usalama wa wilaya kutafuta suluhu ya kudumu ya migogoro baina ya wakulima na
wafugaji.
Okash alitoa ombi hilo jana Novemba 30 wakati wa mkutano
baina yake na Asasi za Kiraia uliolenga
kujadili na kupendekeza mbinu za usuhulishi wa kudumu wa migogoro ya wakulima
na wafugaji wilayani hapa.
“ Pamoja na jitihada kubwa ambazo serikali inafanya kuimaliza
migogoro kati ya wakulima na wafugaji wilayani Mvomero, lakini bado kuna
viashiria vya uwepo wa migogoro baina ya makundi hayo. Nimewaita ndugu zangu wa
Asasi za Kiraia mnaofanya kazi zenu wilayani hapa, ili kwa pamoja tujadili na
kupendekeza mbinu muafaka ambazo zitasaidia kumaliza kabisa migogoro hiyo.
Alisema Okash.
Katika hatua nyingine Okash alizitaka Asasi za Kiraia
zinazofanya kazi wilayani hapa kujielekeza katika kutekeleza miradi ambayo ina matokea
chanya ya moja kwa moja kwa jamii ili kusukumu kwa haraka gurudumu la Maendeleo
ya wilaya ya Mvomero na Tanzania kwa ujumla.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...