Na Pamela Mollel,Arusha
Naibu
Spika wa Bunge la Jamhuri wa Muungano wa Tanzania Tulia Ackson
amekipongeza chuo Cha uhasibu Arusha kwa kutoa aina ya mitaala ambayo
inazingatia umahiri kwa wahitimu na uhalisia wa jamii.
Mhe Ackson ameyasema hayo wakati alipokuwa mgeni rasmi katika mahafali ya 23 ya wahitimu wa chuo Cha uhasibu Arusha .
Amesema
kuwa anakipongeza chuo hicho kwani kinatoa aina ya mitaala ambayo
inazingatia umahiri na utaalamu wa kuwafanya wahitimu kujiajiri lakini
pia kuhudumia jamii kupitia taaluma walizozipata.
Kwa upande
wake Mkuu wa chuo Cha uhasibu Arusha profesa Eliamani Sedoyeka amesema
kuwa matarajio ya chuo Ni kuwa wanatarajia wahitimu hao kutumia
maarifa na ujuzi walioupata chuoni hapo kuhudumia jamii na taifa kwa
ujumla
Alisema kuwa mpaka sasa Chuo hicho kinatoa mafunzo ya kuanzia ngazi ya Astashahada,Stashahada,Shahada na Shahada ya Uzamili
"Mpaka
sasa chuo kinatoa takribani kozi 17 kwa ngazi ya cheti
/Astashahada,kozi kumi na saba ngazi ya Stashahada,kozi kumi na nane
ngazi ya Shahada na kozi kumi na mbili za Shahada ya Uzamili"alisema
Sedoyeka
Aliongeza kuwa chuo hicho kimejipanga kusaidia serikali
kukabiliana na changamoto ya ajira kwa kuandaa mitaala inayoendana na
soko la ajira Kitaifa na Kimataifa katika maeneo ya
Uhasibu,Tehama,Fedha,Uchumi,Kodi,Utawala,Bima,Ukutubi,Utalii,Ugavi na
Ununuzi
"Mitaala yetu inawaandaa wanafunzi kuajiriwa lakini pia
wanaandaliwa kwa namna ambayo wanaweza kujiajiri wenyewe na kutimiza
malengo binafsi na yakitaifa pia"Alisema Sedoyeka
Kwa upande
wake mwenyekiti wa bodi ya chuo Cha uhasibu Arusha dkt Mwamini Tulli
amesema kuwa chuo kinaendelea kutoa mafunzo yenye mitaala ya kuwezesha
wahitimu wajiajiri hivyo kuweza kupambana na soko la Sasa .
Alimpongeza
Mkuu wa Chuo Cha Uhasibu Arusha, Prof. Eliamani Sedoyeka, Menejimenti
ya Chuo na Watumishi wote wa Chuo kwa kazi nzuri waliyofanya ambayo
imefanya Chuo kufikia katika hatua kubwa ya maendeleo
Aidha
alihaidi kushirikiana kikamilifu na kufanya kazi na Uongozi wa Chuo ili
kuhakikisha kwamba mikakati ambayo Chuo kimejiwekea katika utekelezaji
wa majukumu yake ya kutoa mafunzo, kufanya tafiti na kutoa ushauri wa
kitaalamu inatekelezwa ili kulinda hadhi ya Chuo ambayo kimejijengea
hapa nchini
Mwanafunzi bora Anastazia Shayo akifurahia zawadi alizozipata katika mahafali hayo
Katibu Mkuu wa umoja wa vijana wa Chama Cha mapinduzi kenani kihongosi ni mmoja wa wahitimu waliohitimu katika mahafali hayo ya 23
Wahitimu wa chuo cha uhasibu Arusha wakiwa katika mahafali ya 23 jijini Arusha
Mwakilishi wa wahitimu Michael Munichi aipongeza chuo hicho pamoja na wahitimu kwa kufikia hatua hiyo
Kushoto ni Mkuu wa Chuo cha uhasibu Arusha Profesa Eliamani Sedoyeka akiteta jambo na Naibu Spika wa Bunge la Tanzania Tulia Ackson katika mahafali ya 23 ya wahitimu wa chuo cha uhasibu ArushaMkuu wa chuo cha uhasibu Arusha Eliamani Sedoyeka akizungumza na wahitimu katika mahafali ya 23 jijini Arusha
Spika wa Bunge la Tanzania Tulia Ackson akifafanua jambo katika mahafali hayo yaliyofanyika leo jijini Arusha
Mwenyekiti wa Baraza la uongozi wa chuo cha uhasibu Arusha Dkt,Mwamini Tulli akizungumza katika mahafali hayo
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...